Alhamisi, 26 Mei 2022

menstral day

 

kesho ni siku ya kimataifa ya hedhi duniani .

siku hii inaadhimishwa wakati kukiwa na changamoto chungu nzima hasa la ukosefu wa taulo za hedhi.Swala la hedhi linachukuliwa na jamii kuwa ni jambo ambalo halistahili kujadiliwa kwa uwazi.Pia tamaduni za kiafrika liliona kama ni mwiko kwa mwanamke aliyenahedhi kutangamana na wengine,na kuonekana kama mchafu.hivyo basi wasichana wanapovunja ungo wanaona haya kuzungumza na pia changamaoto jinzi ya kuzipata taulo.Wasichana wengi wanaostahili kuwa shuleni hupotesa muda mwingi nyumbani kila mwezi kutokana na hedhi.pia wanatumia njia ambazo sio salama kujizua wanapokuwa kwenye hedhi.Mashirika ya kijamii yamejitokeza kutoa pedi shuleni ilikuhakikisha wasichana hawakosi huhudhuria masomo,pia elimu kuhusu usafi na hedhi inatolewa. Unyanyapa au kutengwa  wakati wa hedhi pia ni changamoto kwa wanafunzi wengi  na ni muhimu kuelimisha jamii kuwa hili ni jambo la kawaida na halina aibu.

Wasichana wanapokosa hela ya kununua pedi,waohujihuzisha na maswala ya ngono za mapema ili wapate namna ya kupata pedi.swala hili huchangia ndoa za mapema. Suala la kupatikana kwa vifaa vya hedhi nalo limekuwa tatizo kutokana na bei yake kuwa juu lakini siku za karibuni baadhi ya nchi zimepitisha taulo za kike kuwa bure au kuondolewa kodi na ushuru kama njia ya kutokomeza umaskini utokanao na hedhi salama. Siku ya hedhi salama huadhimishwa tarehe 28 mwezi Mei kwa kuwa mzunguko wa hedhi kwa mwezi ni siku 28 na mtu anaweza kutokwa na hedhi kwa wastani wa siku 5 au 7 kila mwezi. 

 

Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus-WHO

Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus ateuliwa kuhudumu kwa muhula wa pili.

WHO Director-GeneralNchi Wanachama wa Shirika la Afaya Duniani(WHO) zimemchagua tena Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus kuhudumu kwa muhula wa pili wa miaka mitano kama Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo. Dk Tedros alichaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo 2017.Kuchaguliwa kwake tena kulithibitishwa wakati wa Mkutano wa 75 wa Afya Ulimwenguni huko Geneva,apolikuwa mgombea pekee. 

Dk Tedros akiongea baadaya ya uchanguzi huo,alisema anmefurahi kupewa fursa nyingine kudumu kama Mkurugenzi mkuu wa WHO.Alisema atatekeleza majukumu yake kama inavyohitajika,kushirikiana na mataifa wnanachama,hata kama changamoto ni nyingi. Shirika la afya duniani hushirikiana na nchi wanachama na pia washirika na wadhamini  , ili kuhakikisha dhamira yake ya kuendeleza maswala ya afya, kuhakiki dunia ni salama na kuwahudumia walio hatarini.

Uchanguzi huu unakuja baadaya ya  uchaguzi ulioanza Aprili 2021 wakati Nchi Wanachama zilialikwa kuwasilisha mapendekezo ya wagombeaji wa wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu. Bodi ya Utendaji ya WHO, iliyokutana Januari 2022, ilimteua Dk Tedros kuwania muhula wa pili.Mamlaka mapya ya Dkt Tedros itaanza rasmi tarehe 16 Agosti 2022. Mkurugenzi Mkuu anaweza kuteuliwa tena mara moja, kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Bunge la Afya Ulimwenguni.

Wakati wa muhula wake wa kwanza, Dk Tedros alianzisha Mabadiliko mapana ya WHO, yenye lengo la kuongeza ufanisi wa Shirika katika ngazi ya nchi ili kukuza maisha ya afya, kulinda watu wengi katika dharura na kuongeza upatikanaji wa afya kwa usawa. Pia aliongoza mwitikio wa WHO kwa janga la COVID-19, milipuko ya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na athari za kiafya za majanga mengine mengi ya kibinadamu.Pia alijipata pambaya huku Marekani ikimstumu kwa kuegemea upande wa nchi ya Uchina kuhusiana na maswala ya janga la COVID-19.aliyekuwa Rais waMarekani Donald Trump akionya kutatisha msaada kwa shirika hilo.Marekani ni mfadhiri  mkubwa wa WHO.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk Tedros aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ethiopia kuanzia 2012-2016 na Waziri wa Afya, Ethiopia kuanzia 2005-2012. Pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria; kama mwenyekiti wa Bodi ya Ubia ya Roll Back Malaria (RBM); na kama mwenyekiti mwenza wa Bodi ya Ubia kwa ajili ya Afya ya Mama, Watoto Waliozaliwa na Mtoto.