Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2021

WHO UJUMBE -CHINA

WHO UJUMBE -CHINA Uchunguzi uliosubiriwa kwa muda mrefu ili kujua kiini cha Virusi vya Corona ,Wuhan,China utaziduliwa hivi karibuni. Hii ni kufuatia tanngazo kuwa Wanasayansi kumi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) watatembelea Uchina kutoka Alhamisi. Hii inakuja zaidi ya mwaka mmoja baada ya janga hilo kuanza. Kumekuwa na mashtaka kwamba Beijing imejaribu kuzuia uchunguzikufanyika.   Uchunguzi huu utakuwa muhumi ili kupata uvumbuzi wa chanzo cha janga la coronavirus ambalo limeharibu ulimwengu, na kusababisha vifo vya watu milioni mbili, na pia kupelekea kuzorota kwa uchumi wa ulimwengu.   Ujumbe wa WHO utafanya utafiti wa pamoja na wanasayansi wa China juu ya asili ya Covid-19. Hapo awali, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alikemea namna China ilikuwa ina chelewesha Kuingia nchini kwa dakika ya mwisho ujumbe wake mapema mwezi.   Haya hivyo,Wataalam wa WHO watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili,Beijing.baadaye, wanatarajiwa kutembele...

COVID-19 Kenya

Picha
  COVID-19 Kenya waalimu Huku chanjo dhidi ya Covid -19 ikitarajiwa kutolea baadaye mwezi wa Februari,serikali imesema kuwa   Walimu watapewa nafasi ya kwanza,miongoni mwa wafanyikazi wengine walioko kwenye hatari ya kupata maabukizi ya Covid-19.   Hata hivyo,Wizara ya Afya inasema kuwa wanafunzi hawamo kwenye mpango wa chanjo kwa sababu majaribio ya chanjo ya kliniki kwa watoto bado hayajakamilika. Awamu ya kwanza ya Zoezi la chanjo litalenga watoa huduma muhimu, pamoja na wafanyikazi wa afya na vikosi vya usalama. Wazee na wale walio magonjwa mengine kama kisukali,shinikizo la damu,figo na mengine watapewa kipaumbele .   Tangazo hilo lilitolewa na Katibu wakudumu katika Wizara ya Afya Dkt Mercy Mwangangi Jumatano.   Alisema Kenya imepata dozi zake za kwanza milioni 24 za chanjo kupitia Covax, mpango wa nchi 189 ambao unakusudia kupata na kusambaza chanjo za Covid-19 kwa vikundi vilivyo hatarini ya maabukizi.   Alisema Kenya hadi sasa imejari...

WHO -China Ujumbe

Picha
  China yawazuia wataalam wa afya wa WHO kuingia nchini humo. Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO) limekemea hatua ya Uchina,kuwazuia kuingia nchini humo kwa timu inayochunguza asili ya janga la coronavirus. Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema wanasayansi wawili wa timu ya Umoja wa Mataifa tayari walikuwa wameondoka nchi zao kuelekea Wuhan, walipoambiwa kuwa maafisa wa China hawajapitisha idhini zinazohitajika kuingia nchini.   Dkt.Ghebreyesus alisema alikuwa akiwasiliana na Uchina kabla ya ziara ya wawili hao kuanza, na kila kitu kilikuwa kamili baina yake na China. Akihutubia wanahabari kutoka makao makuu ya shirika hilo,huko geneva,uswizi,Dkt.Ghebreyesus alisema,"Nimesikitishwa sana na habari hii."   "Nimekuwa nikiwasiliana na maafisa wakuu wa China na nimeelezea kuwa ujumbe huu ni kipaumbele kwa WHO na timu ya kimataifa."   azimio la kutaka uchunguzi huru . Tedros alisisitiza kuwa madhumuni ya mkutano huo ilikuwa kut...

Oxford-AstraZeneca

 Chajo ya  Oxford-AstraZeneca Huku chanjo dhidi ya virusi ya Corona yaani COVID -19 ikianza kutolewa kwenye mataifa yalioendelea,kenya inatarajiwa kuanza kutoa chanjo hiyo mwanzoni mwa januari mwaka huu. Hapo awali, Wizara Ya Afya ilitoa taarifa kuwa Shehena ya chanjo ya Covid-19 inatarajiwa nchini Kenya mwezi huu, huku walengwa wa kwanza wakiwa vikundi vilivyo katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi. Isitoshe,Kenya imeagiza   dozi milioni 24 za chanjo ya Chuo Kikuu cha Oxford-AstraZeneca ambayo ni ya bei nafuu na inahifadhiwa kwa urahisi. Baadhi ya walio kwenye hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona ni pamoja na Wafanyikazi wa afya, maafisa wa polisi, wazee na walimu . Chanjo ya Chuo Kikuu cha Oxford-AstraZeneca itatolewa   katika robo ya kwanza ya mwaka huu. Kulingana na Wizara ya Afya watu ambao wanaokuwa kwenye mukushanyiko wa umati na wale walioadhirika na magonjwa mengine ya kiafya watakuwa wa kwanza kupewa chanjo dhidi ya coronavirus. Inakadir...