WHO UJUMBE -CHINA
Uchunguzi uliosubiriwa kwa muda mrefu ili kujua kiini cha Virusi vya Corona ,Wuhan,China utaziduliwa hivi karibuni.
Hii ni kufuatia tanngazo kuwa Wanasayansi kumi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) watatembelea Uchina kutoka Alhamisi.
Hii inakuja zaidi ya mwaka mmoja baada ya janga hilo kuanza.
Kumekuwa na mashtaka kwamba Beijing imejaribu kuzuia uchunguzikufanyika.
Uchunguzi huu utakuwa muhumi ili kupata uvumbuzi wa chanzo cha janga la coronavirus ambalo limeharibu ulimwengu, na kusababisha vifo vya watu milioni mbili, na pia kupelekea kuzorota kwa uchumi wa ulimwengu.
Ujumbe wa WHO utafanya utafiti wa pamoja na wanasayansi wa China juu ya asili ya Covid-19.
Hapo awali, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alikemea namna China ilikuwa ina chelewesha
Kuingia nchini kwa dakika ya mwisho ujumbe wake mapema mwezi.
Haya hivyo,Wataalam wa WHO watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili,Beijing.baadaye, wanatarajiwa kutembelea Wuhan - mji ambao virusi vya mauti viligunduliwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa 2019.
Asili ya virusi
Amerika na Australia wamekuwa kwenye mtari wa mbele kutoa wito wa kimataifa wa uchunguzi huru juu ya chimbuko la virusi, na kuiweka China chini ya shinikizo kubwa la uwajibikaji.
Pia,Beijing imekabiliwa na ukosoaji wa kimataifa juu ya ukosefu wake wa uwazi wakati wa mlipuko wa mwanzo.
Wataalam watachunguza jinsi virusi viliruka kutoka kwa wanyama kwenda kwa wanadamu ili kuzuia janga jinginekutokea.Lakini udhibiti mkali unaotolewa na Uchina kuhusu utafiti wake wa kisayansi unadidimiza kupata suluhu kamili.
Ni wazi kuwa virusi viliibuka mwishoni mwa 2019 kwenye soko moja huko Wuhan ambapo wanyama wa porini waliuzwa kama chakula.
Jaribio la kugundua asili yake pia limekumbwa na nadharia za njama - iliyoongezwa na Rais wa Merika Donald Trump - kwamba ilivuja kutoka kwa maabara ya virolojia ya Wuhan.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni