Jumatano, 6 Januari 2021

COVID-19 Kenya

 

COVID-19 Kenya waalimu

Huku chanjo dhidi ya Covid -19 ikitarajiwa kutolea baadaye mwezi wa Februari,serikali imesema kuwa  Walimu watapewa nafasi ya kwanza,miongoni mwa wafanyikazi wengine walioko kwenye hatari ya kupata maabukizi ya Covid-19.


 Hata hivyo,Wizara ya Afya inasema kuwa wanafunzi hawamo kwenye mpango wa chanjo kwa sababu majaribio ya chanjo ya kliniki kwa watoto bado hayajakamilika.

Awamu ya kwanza ya Zoezi la chanjo litalenga watoa huduma muhimu, pamoja na wafanyikazi wa afya na vikosi vya usalama.

Wazee na wale walio magonjwa mengine kama kisukali,shinikizo la damu,figo na mengine watapewa kipaumbele .

 Tangazo hilo lilitolewa na Katibu wakudumu katika Wizara ya Afya Dkt Mercy Mwangangi Jumatano.

 Alisema Kenya imepata dozi zake za kwanza milioni 24 za chanjo kupitia Covax, mpango wa nchi 189 ambao unakusudia kupata na kusambaza chanjo za Covid-19 kwa vikundi vilivyo hatarini ya maabukizi.

 Alisema Kenya hadi sasa imejaribu zaidi ya watu milioni moja dhidi ya  Covid-19 na imeweka mikakadi madhubuti kuzuia maambukizi ya coronavirus baada ya shule kufunguliwa Jumatatu wiki hii,nchini.

Hapo awali,Bi Henrietta Fore Mkurugenzi wa Shirika la umoja wa mataifa la watoto(UNICEF) alitaka selikali pia kutoa chanjo kwa wanafunzi na waalimu,ili kuzuia madhara kwenye sekta ya elimu.

Hata hivyo alisema uamuzi wa hatua hiyo uko mikononi mwa serikali husika.

 Takwimu zinaonyesha kuwa watoto hubaki bila dalili. Watoto kati ya miaka mitano na 19 hawako katika hatari kubwa ya kuambukizwa Covid-19 lakini wanaweza kubeba virusi na wanaweza kuambukiza watu wazima.

 Kenya ina zaidi ya walimu 340,000 wanaofanya kazi chini ya Tume ya Huduma ya Walimu (TSC) na karibu wengine 160,000 wanaofanya kazi katika shule za kibinafsi.

 Kumekuwa na hofu ya kuambukizwa kwa wingi mashuleni baada ya kufunguliwa Jumatatu baada ya fungwa tangu Machi mwaka jana.

kulikuwa na visa kadhaa vya walimu ambao walipata virusi hivyo na vifo vingine viliripotiwa,baadaya taasisi zilipofunguliwa mnamo Oktoba,mwaka jana.

 Kulingana na Dkt. Mwangangi Kenya itategemea sana chanjo ya AstraZeneca kwa sababu ya kubadilika kwake kwa mifumo ya sasa ya kuhifadhi baridi nchini.

 Pfizer na Moderna pia wameanzisha chanjo za Covid-19 lakini hizo zinahitaji kuhifadhiwa kwa joto la chini sana.Alitangaza kuwa wizara yake, pia itasambaza programu ya simu ya rununu,ijulikanayo kama M-Dharura ili kupata taarifa na pia kutoa habari kuhusu kesi za Covid-19.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni