Uterine Fibroid Embolization
Uterine Fibroid Embolization Je wajua kuwa ugonjwa wa fibroids yaani uvimbe au vivimbe ambavyo huwa kwenye ukuta wa kizazi (uterus) waweza kutibiwa na mwanamke akawa hana matatizo tena kwenye uzazi wake? Kwa mujibu wa daktari, Timona Obura, ambaye ni mtaalam (Gynaecologist) katika hospitali ya Aga Khan, Hii inawezekana kutokana na tecnhologia ya kisayansi ambayo inajulikana kama Uterine Fibroid Embolization. Vivimbe hivyo vinaweza kuwa vidogo Kama ncha ya kidole au vikubwa Kama viasi .Pia vinaweza kugunduliwa, kwa kutumia tecnologia inayojulikana kama Ultrasound. Mwanamke anaweza akawa kwenye hatari ya mimba kutoa(miscarry) kwani,uvimbe unaweza kujaa kwenye sehemu anayokaa mtoto. Ingawa kuna aina za upashuaji zinazotumiwa kuondoa Fibroids,Daktari Obura anasisitiza kuwa Embolization ni namna maalum ambayo haihitaji upasuaji wa kawaida.Pia hamna madhara kama upasuaji wa kawaida. Hapa mwanamke au mgonjwa anaelimishwa kuhusu jinsi upasuaji unav...