Trachoma
Trachoma (Vikope) Trachoma au vikope ni ugonjwa unaosababisha upofu.isitoshe,maabukizi yake yanatokana na bakteria aina ya Klamidia Trakomati. Ugonjwa huu unaweza kuthibitiwa ukitibiwa mapema. Mazingira machafu na ukosefu wa maji safi huchangia maabukizi ya maradhi haya. Nchini kenya jamii za wafungaji wa kuhamahama huadhrikika Zaidi. Hata hivyo idadi ya magonjwa imepungua kwa asilimia 91 kote duniani Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya watu walio kwenye hatari ya maabuziki imepungua kutoka 1.5 billioni mwaka wa 2002 hadi 142 millioni mwaka 2019. Tafiti zinaonyesha kuwa ,kati ya nchi 44 ambazo ziko Afrika na Asia, zilikubwa na ugonjwa huu lakini umethibitiwa kwa kiwango cha juu kwa sasa. WHO inasema kuwa, idadi ya waliohitaji upasuaji kurekebisha hali ya upofu ya trachoma imepungua kutoka millioni 7.6, mwaka 2002 hadi millioni 2.5 mwaka 2019. Mbali na hayo,serikali ya Kenya imeweka mikakati ya kuto...