Chakula salama ni jukumu la
kila mmoja
Leo ni siku ya usalama wa chakula duniani.
Huku siku hii ikiadhimishwa kote duniani ni jukumu ya kila
mmoja kuhakikisha chakula anakinunua na kula ni salama kwa matumizi.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani (WHO)Dkt Tedros
Adhanon Ghebreyesus anasema hii ni fursa muhimu kuhamasisha juu ya hatari za
chakula kisicho salama kwa wote hususan serikali,wazalishaji na watumiaji .
Hivi karibuni kumekuwa na
taarifa kuwa chakula kinacholiwa nchini Kenya kina kemikali ambazo husababisha
maradhi kwa watu.
Zina viwango za juu Zaidi ya ilivyohalalishwa na shirika
la afya duniani.
Kwa mfano kilo moja ya mboga hizo ilifanyiwa utafiti
katika maabara za KEPHIS na ile ya kibinafsi ya ANALAB .Matokeo ya sampuli
kutoka maduka inaonyesha zilikuwa na 0.13mg kwa kila kilo na 0.15 kwa kila kilo
ya zebaki, ambayo ni Zaidi ya viwango vilivyo ratibiwa na kuidhinishwa na
shirika la afya duniani vya 0.1 kwa kila kilo.
Ripoti pia inaonyesha kuwa mboga kutoka masoko ya
korogocho ilirekodi kiwango cha juu cha zebaki cha 0.11 .Imedainika kuwa kila
mwaka watu zaidi ya milioni 600 huadhilika kwa
kula vyakula vilivyo na chemikali na madini yenye sumu huku wengine 42,000
wakifariki kila mwaka.
Hali hii pia uchangia pakubwa
kuzorota kwa uchumi ,biashara na sekta ya utalii
Zaidi ya hayo,takwimu za Mashirika ya umoja
wa mataifa yanayohusika na afya,chakula na kilimo zinakadilia takribani dola
bilioni 95 zinazopotea kila mwaka kutokana na chakula kisichofaa kwa nchi
zinazoendela .
Ni jukumu la mataifa kuhakikisha
chakula kimelindwa .
Pia ni wajibu wakila mmoja kuchukua hatua muafata kuona kua
usalama wa chakula umedumishwa.
Wanaukuza chakula ,wauzaji na
wanaokula hicho chakula wana majukumu yakulinda chakula,kwani chakula
kisafi,afya njema.
Madini haya hupatikana kwenye maji yanyotoka
viwandani vya magari,rangi na wakati yanatumiwa maji hayo husababisha mimea
kuwa na viwago vya juu vya madini na kemikali zenye sumu.
Hatua madhubuti zichukuliwe
kuhakikisha chakula kimedhibitiwe na serikali kuhakikisha ni salama.
Tekinologia ya kisasa ya kudhibiti
chakula ili kuhakikisha ni salama ;inahitajika.
Serikali pia zinamajukumu ya
kuwaelimisha wananchi jinsi ya kutunza mazingira ili kuepukana na hatari za
chakula chenye sumu.
Ni muhimu kujiepusha kununua vyakula vya mitandao ambayo
asili yake si hakika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni