Ijumaa, 7 Juni 2019

magonjwa ya zinaa


Maambukizi ya magonjwa ya zinaa ya ongezeka

Magonjwa ya zinaa yaongezeka, huku takwimu zikionyesha kuwa kuna maambukizi ya Zaidi ya millioni moja kila siku.

Kwa mujibu wa Shirika la afya ulimwenguni, WHO.
Waadhiriwa wa maradhi ya zinaa ni watu wa umri wa miaka 15 hadi 49.

Magonjwa hayo ni kama vile,kisonono,kaswende ,trichomoniasis na klamidia

Isitoshe,endapo maradhi haya yataendea bila kutibiwa ,yanaweza kuwa na adhari katika afya ya mwadhiriwa.

Wataalamu wa afya watapendekeza umuhimu wa kuchukua hatua za kukinga au kuzuia maradhi ya zinaa.

NI jukumu la kila mgonjwa kutafuta na kupata matibabu ili kudhibiti magonjwa ya zinaa.

Magonjwa haya yanaadhari katika maisha ya anayeugua.

Kukosa au kupoteza ujauzito, watoto kufia tumboni kwa akina mama na pia hatari ipo kuambukuzwa HIV.

Wataalamu wa afya wa WHO wnadokeza kuwa mtu mmoja kati ya 25 duniani kote ana aina moja ya maradhi ya zinaa.

Huku wengine wakiwa na maabukizi ya magonjwa Zaidi kwa wakati mmoja.
Takwimu za mwisho kuchapishwa na WHO mwaka wa 2012 zinaashiria kuwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa yanazidi kuongezeka kila uchao.

Matokeo ya utafiti wa kimataifa wa WHO kwa mwaka 2016 umeonyesha hali inaendelea kuwa mbaya.

Kuna maambukizi Zaidi. Kuna visa milioni 127 kwa ugonjwa wa klamidia, huku kisosnono kikiwa na visa milioni 87 na kaswende visa milioni 6.3. 

Hali hii ikichangia vifo vya watoto wachanga kuongezeka kote duniani.Watoto takribani 200,000 kufa kabla kuzaliwa.

Zaidi ya hayo,wito umetolewa kwa kina mama wajawazito kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara hasa kwa maradhi ya kaswende na HIV ili kupunuza vifo zaidi
Hata kama inaaminika magonjwa haya yana tiba, changamoto iiliyopo kwa sasa ni upungufu wa dawa aina za benzathine penicillin zinazotibu hasa kaswende.

Dalili

Dalili hutofautiana baina ya wnawake na wanaume.
Wanaume huona dalili za maradhi ya zinaa siku chache baada ya kushiriki ngono huku akina mama hukukua muda mrefu; wiki au miezi baada ya kuambukizwa.

  • ·       Kutoka usaha kwenye njia ya haja ndogo
  • ·       Kusikia maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo
  • ·       Kutokwa na uvimbe au vidonda sehemu ya uke au ya ume
  • ·       Kutokuwa na hamu ya kushiriki ngono.
  • ·        Kuvuja damu kabla ya muda wa hedhi

Matumizi ya mipira ya kondom wakati wakushiriki ngono yanapendekezwa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni