Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani,
Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus,azuru Uganda kutadhimini hali ilivyo kwa
sasa,baada ya mripuko wa Ebola huko Kasese, Uganda.
![]() |
WHO photo |
Kwenye taarifa, Mkurugenzi mkuu alitoa
hakikisho kuwa shirika lake litajitahidi kuhakikisha kuwa ugonjwa wa Ebola
umekabiliwa.
Alisema hali sio nzuri, hadi ugonjwa wa
Ebola ukabiliwe Congo.
Hata hivyo alisema kuna mafanikio ya
kupungua kwa maradhi hayo hasa Butembo na katwa.
Isitoshe, kwenye kikao katika nchi hizo
mbili,alitilia mkaso kuwa endapo idadi ya maabukizi ya Ebola yamepungua, si
vema kuweka Imani kuwa hali iko sawa.
Alisema sehemu ya Mabalako ambapo
ugonjwa huu ulipolipuka mara ya kwanza
mwaka wa 2018,imekuwa ni sehemu ambapo milipuko Zaidi imeripotiwa.
Hii pia ni sehemu watu waliopatikana na
Ebola Uganda walitokea.
Nchi za Uganda na Kenya zimeweka
tahadhari mipakani tangu kuzuka kwa ebola na kifo cha kijana mmoja aliyetokea
huku Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wiki moja iliyopita.
![]() |
Photo PPU |
Baadaye Dkt Ghebreyesus,akiadamana naWaziri wa Afya na maafisa wa afya alikutana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Mseveni kuhusu tishio la Ebola Uganda.
Alipongeza Uganda kwa hatua walizochukua kufuatia mlipuko wa ebola hivi majuzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni