Rais
Mstaafu Daniel T Moi Aaga Dunia
Mzee Moi ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 95
katika hospitali ya Nairobi alipokuwa amelazwa tangu mwezi wa kumi mwaka jana.
Kundi la madaktari likiongozwa na Daktari wake wa miaka
mingi, David Silverstein limekuwa likimpa mkatibabu kwa matatizo
yanayojirejeeza na kumfanya kusalia kitandani kwa miezi mitatu.
Hali ya afya ya
mzee Moi ilidorola Mwezi uliopita huku madaktari wake wakilazimika
kumrejesha Moi katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Kifo chake alfajiri ya leo kimetangazwa na Rais uhuru Kenyatta
ambaye ni mwanafunzi na mwanawe wa kisiasaAwali,msemaji wake Lee Njiru
alisema Moi alikuwa amekwenda hospitali kwa ukaguzi wa kawaida wa afya
lakini tangu wakati huo,amekuwa ndani nan je ya hospitali.
Mzee Moi, alijeruhiwa kwenye goti alipohusika
kwa ajari iliyohusisha gari lake mwaka wa 2006 huko Limuru .
Kama mwandishi wa maswala ya afya nitamkubuka Rais Moi kama
kiongozi aliyejari afya na malezi bora kwa watu hasa watoto .Alihakikisha
watoto walipata maziwa ya bure shuleni.
Pia
alitilia mkazo mpango wa uzazi kwa akina na mama kwa minajiri ya afya bora na
malezi mema.
Kuhusu
mazingira,Moi aliweka sera kuhakikisha wakulima wamepata miti ilikuzuia
momonyoko wa udongo.
Alikuwa
kwenye mstari wa mbele pia katika maswala la dini.
Rais
alikuwa mkarimu, alipozuru sehemu tofauti za nchi aliwatunuku akina mama na
watoto waliojitokeza kumlaki.
Mola
ailaze roho ya Marehemu Rais Daniel Toritich Arap Moi palipo watakatifu wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni