Alhamisi, 27 Februari 2020

COVID -19 Kenya



Image result for kenya control coronavirusHuku ugonjwa wa Virusi vya Corona –COVID-19 ukiendele kuenea kwa kasi nje ya uchina ,Serikali ya Kenya imelaumiwa kwa kuruhusu kuingia nchini watu  239  warioabiri ndege ya Uchina.Inadaiwa kuwa abiria hao  walitakiwa wasikaribiane au wajitenge na watu kwa muda furani kama tahadhari dhidi ya kuambukiza wa Virusi vya Corona .
Hata hivyo kuna hofu kuwa huenda kunauwezekano kuwa mmoja au zaidi ya abiria wakawa na virusi hivyo ambavyo huchukua wiki kabla dhariri zake kuibuka.
Image result for kenya minister health coronaUgonjwa huu umewauwa maelfu ya watu nchini uchina na pia mataifa mengine nje ya Uchina yameadhirika.
Uchina umekuwa kitovu cha virusi, na kufikia sasa watu 81,291wameambukizwa vurisi hivi ulimwenguni kote na kuwauwa 2,770, wengi wao wakiwa katika taifa la Asia.
Image result for corona virusVirusi vya Corona ambao umepewa jina rasmi Covid-19, mara nyingi huenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mtu.
Serikali kwa upande wake imesema hakuna haja ya kuhofia maambukizi kwani mikakati dhabiti imewekwa kuhakikisha hakuna mtu atakayeingia nchini bila kukaguliwa au kuchunguzwa iwapo ana virusi au la.
“Hatua zote za tahadhari zimewekwa na kila mtu anayekuja nchini hupimwa vya ipasavyo na watalamu wa afya.
Awali serikali ilisema kuwa mipaka na viwanja vya
ndege na pia bandarini hali imedhibitiwa.
Hata hivyo wakenya hawajaridhishwa na hatua ya serikali ya kutowarejesha wakenya 91 waliokwama nchini uchina.
Familia za wahusika sinasema kuwa wapendwa wao wamo hatarini yakuambukizwa virusi na pia kuadhirika kimawazo maana hawatoki nje na pia kuna upungufu wa chakula.
Kufikia sasa visa 15 vimefanyiwa tafiti kwenye mahabara kuhakikisha kuwa watu wote walioonyesha dalili za Corona wako salama.
·         Pia Mipango ya kuhamasisha umma kuhusu jinsi ya kukambiliana na virusi vya Corona endapo vitaripotiwa imewekwa.
·         Kitengo cha dharura chenye maafisa wenye majukumu ya kufatilia na kuchunguza kisa chochote kinachorioptiwa  nchini
·         Vifaa vya kutosha kuwekwa kwenye vituo maalum vya kuchunguza virusi kwa wasafiri wote wanaoingia nchini kutoka mataifa mbalimbali.
·         Mafunzo kwa maafisa wa afya huku maafisa mia tano wakifunzwa katika vituo vya afya vya umma na pia vya kibinafsi.
·         Wananchi wameshauriwa kuwashiriana na Wizara ya Afya kuripoti kisa chochote kinachshukiwa kuwa cha Corona.
Shirika la Afya Duniani lasema dunia sharti ijiandae kukambili na janga la virusi vya Corona
Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema Virusi vya Corona vinaweza kuwa janga




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni