Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya saratani ya muua Njenga Karume

Njenga Karume aaga dunia

Picha
Marehemu Njenga Karume  Aliyekuwa waziri wa ulinzi na mbunge wa zamani wa Kiambaa, Njenga karume amefariki dunia. Karume ameaga dunia katika hospitali ya Karen hapa Nairobi ,alipokuwa akipokea matibabu, baada ya kuugua saratani. Marehemu Karume amefariki akiwa na umri wa miaka 83. Rais Mwai Kibaki ametoa salamu zake za rambi rambi kwa jamaa na marafiki wa Marehemu huku akisema amempoteza rafiki wa dhati. Karume alikuwa kigogo wa siasa na alimuunga mkono rais Mwai Kibaki katika juhudi zake za kuimarisha siasa za chama cha Democratic party(DP). Karume alikuwa mwanabiashara mashuhuri ambaye alikuwa na bidii kama za mchwa.Alijizatiti kuwa mmojawa   matajiri watajika hapa nchini,licha ya kuanzia chini sana. Katika kitabu chake, alichoandika kuhusu maisha yake, Karume alisema vile alijitahidi kutoka uchomaji wa makaa hadi dhahabu. Anatajwa pia kama aliyepigania uhuru, aliyehakikisha tamaduni zinahifadhiwa. Alikuwa mbunge wa kiamba lakini 2007 alipoteza kiti ...