Marehemu Njenga Karume |
Aliyekuwa waziri wa ulinzi na mbunge wa zamani wa Kiambaa, Njenga karume amefariki dunia.
Karume ameaga dunia katika hospitali ya Karen hapa Nairobi ,alipokuwa akipokea matibabu, baada ya kuugua saratani. Marehemu Karume amefariki akiwa na umri wa miaka 83.
Rais Mwai Kibaki ametoa salamu zake za rambi rambi kwa jamaa na marafiki wa Marehemu huku akisema amempoteza rafiki wa dhati.
Karume alikuwa kigogo wa siasa na alimuunga mkono rais Mwai Kibaki katika juhudi zake za kuimarisha siasa za chama cha Democratic party(DP).
Karume alikuwa mwanabiashara mashuhuri ambaye alikuwa na bidii kama za mchwa.Alijizatiti kuwa mmojawa matajiri watajika hapa nchini,licha ya kuanzia chini sana.
Katika kitabu chake, alichoandika kuhusu maisha yake, Karume alisema vile alijitahidi kutoka uchomaji wa makaa hadi dhahabu.
Anatajwa pia kama aliyepigania uhuru, aliyehakikisha tamaduni zinahifadhiwa.
Alikuwa mbunge wa kiamba lakini 2007 alipoteza kiti chake, aliposhindwa na mbunge wa sasa mheshimiwa Stanley Githunguri.
Alikuwa pia mwanzilishi wa kundi la Gikuyu Embu Meru Association(GEMA) na mstahiki mzee wa jamii ya Gikuyu.
Wiki mbili kabla ya kifo chake uvumi ulienezwa kuwa Karume alikuwa amefariki.Kufuatia uvumi huo Rais Kibaki alimtembelea nyumbani kwake huku Cianda, Kiamba katika jimbo la Kiambu.
Mungu ailaze roho yake Karume pema peponi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni