Wakenya wa tambaka mbalimbali waendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa waziri wa mazingira John Njoroge Michuki aliyefariki dunia jumanne,kwa mstuka wa moyo, katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan.
Akizaliwa 1932 katika kitongoji cha Jimbo la Kagema katika wilaya ya Muranga.
Alipata masomo yake ya upili katika shule ya Mangu pamoja na rafikiye wa dhati rais Mwai Kibaki.
Aliendelea na masomo yake katika chuo cha Worcester,Oxford huko Uingereza.
Wengi wamemtaja michuki kama kiongozi mchapa kazi , aliyedumisha nidhamu ya hali ya juu kazini na aliyejitolea kwa kila alilofanya.
Rais Mwai Kibaki ambaye ni rafikiye marehemu alisema kuwa Michuki alikuwa mwanasiasa hodari,aliyetekeleza kazi yake kwa uadilifu.Pia mwana biashara stadi.
Kulingana na mhariri wa habari wa kujitengemea Onesmus Kilonzo Michuki atakubukwa kwa kulainisha sekta ya matatu,na uhifadhi wa mto Nairobi miongoni mwa mengine
“kila ofisi aliohudumia ilipata ufanisi mkubwa.Wengi watamkumbuka milele kwa ukakamavu wake wa utenda kazi”,alisema Kilonzo.
Wabunge jana wariahirisha shughuli za mbunge kuomboleza kifo cha mwenda zake Michuki.Kila aliye nena alimumiminia sifa Michuki na kusema kuwa ameacha pengo ambalo kwa hakika halitazibika.
Mbunge wa Gichungu Martha Karua ambaye pia ni mgombeaji wa kiti cha urais alisema endapo alitofautiana kisiasa na marehemu, Michuki alikuwa kiongozi mwenye hekima na ukakamavu wa hali ya juu.
Mbunge Amina Abdalla pia alimtaja kama baba aliyewataka vijana watie bidii katika lolote wafanyalo.
Wengine waliomsifu michuki ni pamoja na wakuu wa shirika la mazingira duniani UNEP waliosema kuwa alionyesha ubunifu na makini katika maswala ya mazingira.
Baadaye jioni makamu wa rais kalonzo musyoka ,spika wa mbunge Kenneth Marende na baadhi ya wambunge walitembelea familia ya michuki nyumbani kwake Ridgeways.
Rais Kibaki ametatangaza kuwa kupeperushwa kwa bendera nusu mlingoti kwa heshima ya mwenda zake Michuki.
Michuki atazikwa siku ya jumanne huko Kagema.
Mungu amlaze mahali pema peponi.
Marehemu John Michuki |

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni