Jumatatu, 27 Februari 2012

Mzee Nelson Mandela apata matibabu

Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini mzee Nelson Mandela aendelea kupata nafuu baada ya kutoka hospitalini , alikolazwa kutokana na maumivu ya tumbo ambaye yamekuwa yakimtatiza kwa muda mrefu.

Hapo awali, taarifa kutoka ofisi ya Rais Jacob Zuma ilisema Mzee Nelson Mandela alilazwa hospitalini na akawaomba  Waafrika Kusini kumuombea nafuu ya haraka.

Mzee Mandela, mwenye umri wa miaka 93 hajaonekana hadharani kwa muda mrefu sasa kufuatia kudorora kwa afya yake .

Wananchi wengi nchini Afrika Kusini walipokea habari za kulazwa kwake hospitalini kwa hofu na huzuni tele, lakini wakasema wanaendelea kumuombea apate afueni ya haraka.

Mbali na hayo,mzee Mandela aligunduliwa  kuugua saratani ya tezi dume,2001 na baada ya matibabu akapona, kwani iligunduliwa mapema.

Alikuwa Rais wa kwanza mweusi katika nchi hiyo kuanzia mwaka 1994 na kisha akaachia ngazi mwaka 1999.

Mandela anatambulika kote duniani kwa juhudi zake za kupambana na utawala wa kibaguzi wa Makaburu kwa muda mrefu na baadaye kuikomboa Afrika Kusini kutoka mikononi mwa wabaguzi hao wa rangi katika muongo wa tisini.


Pia sisi hapa nchini Kenya tunashukuru Mola kwa kumlinda mzee Mandela na pia tunamuombea ampate afueni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni