Jumatatu, 20 Februari 2012

WHO yasema depo provera ni salama



Shirika la Afya Duniani ( WHO) limeondolea lawama shindano ya Depo Provera kuwa inachangia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Shirika hili (WHO) linahakikishia  wanawake wanaotunia aina ya uzazi wa mpango wa homoni kuwa hakuna hatari ya kutumia aina hii, kama ilivyo daiwa hapo wali.

Hata hivyo (WHO) imeonya  kuwa  ni aina moja pekee ya uzazi wa mpango inayozuia maambukizi ya Virusi  Vya Ukimwi - kondomu au mpira.

Huku likisisitiza kuwa ni muhimu kwa wale wako kwenye hatari ya kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi kuchukua tahadhali.

Zaidi ya hayo, Shirika la Afya Duniani utafiti unafanywa kwa nia ya kuhakikisha malengo ya milenia ya afya imefikiwa.
Uvumbuzi kuwa utumiaji dawa ya upangaji uzazi ya homoni ijulikanayo kama Devo Provera unachangia ongezeko la maabukuzi ya ugonjwa hatari wa ukimwi, miezi michache iliyopita, uliwaacha wanawake wengi na hofu na husuni tele.
Inakadiriwa kuwa takribani millioni 12 ya wanawake wenye umri wa kati ya  miaka 15 na 49 katika Afrika kusini na Jangwa la Sahara wanatumia homoni za kuzuia mimba(Depo provera).

Takwimu hizi zilitolewa na shirika moja la afya la Marekani lililofanya utafitia uliochapishwa  na jarida la The Lancet.

Shirika hili la afya, lilitoa tahadhali kuwa  akina mama wanaotumia aina ya uzazi  upangaji wa homoni(Depo Provera) wako  hatarini ya kuambukizwa au kuwaambukiza waume wao Virusi Vya Ukimwi ,kuliko wale wasiotumia aina hii.

Kufuatia utafiti huu,Shirika la Afya Duniani (WHO) liliitisha kikao cha dharula Januari mwaka huu (2012) ili kutadhimini iwapo ushahidi huu unatosha kuwashauri wanawake kuachana na aina hii ya mpango wa uzazi ili kukomesha maambukizi zaidi.

Kutokana na matokeo haya, ni vyema kwa yeyote anayetumia aina yeyote ile ya mpango wa uzazi kufahamu kuwa, endapo kundomu haitumiwi panapo hatari ya maambukizi, basi yule mwanamke au mwanaume atakuwa akihatarisha maisha yake.
Kuzuia ni bora kuliko kuponya.

Ni jukumu ya kila mtu kuhakikisha analinda afya yake kutokana na mikasa ya kujitakia, kwani mkasa wa kujitakia hauna kilio.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni