Ijumaa, 21 Juni 2019

ugonjwa wa kifafa


David Kamau ni mkaazi wa Mowlem viungani vya jiji la Nairobi.
Toka utotoni yeye anaishi na ugonjwa wa kifafa.Kwa muda mrefu,wazazi wake walitafuta tiba za kienyeji kwa waganga wa kienyeji bila mafanikio.

Walisema mtoto wao amefanyiwa uchawi ila hawakufahamu kuwa aliugua kifafa.
Mara kwa mara Kamau alipoteza fahamu na kuzimia,alianguka na akapoteza muda mwingi kutafuta tiba.Hakuendelea na masomo yake baaada ya kidato cha nne.

Kamau ni miongoni mwa watu robo tatu walio na ugonjwa wa kifafa katika nchi zenye kipato cha chini , na ambao hawapati matibabu wanayoyahitaji.

Hii inachangia kuwepo hatari ya kufa kabla ya wakati wao. Kulingana na  ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO baadhi ya wagonjwa wa kifafa hawapati matibabu inavyostahili.

Zaidi ya hayo wengine wanaogopa kwenda hospitalini kwa sababu ya unyanyapa,na pia Imani potovu zinazohuzishwa na ugonjwa huu.

WHO inasema endapo wagonjwa wangepata matibabu na kwa haraka hali yao ya kiafya ingekuwa bora.

WHO inasema pengo la ukosefu wa matibabu au huduma za afya karibu na waathiriwa linaweza kizibwa .Asili mia 70 wana kifafa.

Inasema kuwa hali si sawa katika mataifa yenye chumi ndogo ikilinganishwa na mataifa yaliyostawi kiuchumi.Vifo vya mapema ni Zaidi katika nchi zenye chumi ndogo.Watu wenye kifafa wanakunwa na magonjwa mengine ya kiakili na hii inashababisha kuzorota kwa hali ya mtu.

WHO inakadiria kuwa kuna wa millioni mia tano (500) wenye kifafa kote duniani.
Nchini kenya hali sio tofauti .Watu millioni moja wana kifafa huku wawili kati ya mia hawajapata tiba au hawafahamu kuwa wana hali hii.

Watu  millioni 2.4 hupatikana na kifafa duniani kote kila mwaka.
Vifo hutokea hasa wakati mtu anapozama maji,majeruhi ya kichwa au kuchomeka mtu anapopata mshtuko.

Jinsi ya kumsaidia mtu anapopata mshtuko wa kifafa.             
  • Unastahili kushikilia kichwa cha mgonjwa
  • Kichwa kinapaswa kugeuswa kwa upande
  • Usijaribu kufungua kinywa au kuweka kijiti au kijiko
  • Endapo shambulio litapita dakika tano,unapaswa kutafuta ambulensi kwa dharula.
  • Asipewe chakula wala maji
  • Shambulio hudumu dakika 2-3 kwa kawaida.
  • Usimuamushe hadi apate fahamu

Hali ikizidi tafuta usaidizi wa mtaalam wa afya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni