Ukeketaji
ni kuondoa sehemu ya nje ya uke na katika tamaduni na mila za jamii zingine ni
kuondoa sehemu yote na kuishona.
Ni
kufuatia hatua hii Rais wa Kenya ,Uhuru Kenyatta akiongea katika kongamano la
usawa wa jinsia inayoendele nchini Canada Rais wa kenya uhuru Kenyatta amesema Kenyaiko
katika mstari wa mbele kutokomesha upasaji tohara.
Mikakati
pia imechukuliwa kuhakikisha ndoa za mapema zimekomeshwa huku masomo ya shule
ya upili yakiwa ni lazima kwa kila mtoto kuhudhuria.
Alisema
hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mzazi au mtu yeyote atakaye zuia au
kumkataza mtoto haki yake ya masomo.
Swala
la ukeketaji limekua changamoto hapa nchini Kenya na Bara la Afrika kwa jumla.
Mila
ya ukeketaji imekidhiri katika sehemu tofautia nchini Kenya.Hata baada ya kupigwa
marufuku,wengi ufanya tendo hili ,japo kwa usiri.
Majimbo
ya Migori,Meru,Taita taveta,Kisii ,Narok,Kajiado na pia Kaskasini Mashariki na
Pwani yakiadhirika Zaidi.
Ukeketaji
hutofautiana na tamaduni na mila za
kabila lakini lengo ni kuhakikisha au kulinda mwanamke katika matamanio yake ya
kujamiiana.
Tishio
hili limesababisha akina mama kuwa hatarini hasa wakati wanapojifungua;wanapata
matatizo ya kisaikolojia.
Wanawake
huchekwa na walio kwenye ndoa hudharauliwa na kukejeriwa na wanawake wenzao
waliokeketwa.
Kumekuwa
na matukio ambapo akina mama walioolewa kulazimishwa kukeketwa .Mara kwa mara
wao hufumaniwa wanapotuka katika shughuli zao za kila siku.
Kulingana na takwimu za shirika la afya
Duniani WHO,wasichana na akina mama Zaidi ya millioni 200 wamekeketwa huku
wengine millioni 3 wakiwa kwenye hatari za kukeketwa.Wao wako kwa umri wa miaka 15 hadi 49.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni