Jumanne, 11 Juni 2019

male contraceptive gel -mpango uzazi



Dawa ya kupanga uzazi kwa wanaume kufanyiwa majaribio katika hospitali kuu ya Kenyatta nchini Kenya.

Kulingana na mila na tamaduni za kiafrika kupanga uzazi ni mwiko.
Hata hivyo desturi na tamaduni hizi zimepitwa na wakati;ijapo kukuwa wachache wamezifuatilia na kuziheshimu.

Zaidi ya hayo maswala ya upangaji uzazi kwa wanaume yanazungumziwa kwa siri sana.
Kasuba ilioko ni kuwa uzazi mpango ni majukumu ya akina mama.
Lakini baadhi ya wanawake wanaotumia aina tofauti za mpango uzazi wanakabiliwa na changamoto za afya.

Wao hupata maradhi yanayotokana na mayumizi ya aina mbalimbali za mpango uzazi.

Hivyo basi watafiti na wataalam wa afya wamebuni mbinu mpya ya kuhakikisha kuwa swala la uzazi mpango ni jukumu la kina mama pekee.Wanaume pia wapaswa kujumuishwa kwenye shughuli hii muhimu.
Ni kufuatia tafiti hii,hospitali ya Kenyatta na chuo kikuu kimoja kutoka Marekani imezidua utafiti wa dawa ya kupanga uzazi kwa wanaume.
Dawa hii itatumiwa kupaka katika sehemu ya kusoto ya mbega  kwa muda wa wiki 40.
Pia mbegu za kiume zitachukuliwa kufajiwa uchunguzi wa kiafya.Huku jaribio hili likitarajiwa kuchukua wiki 4(nne) hadi 8 (nane).
Mpango huu unatumainiwa kuchukua muda wa miaka miwili kupata mapokeo mwafaka.

Watakaoshiriki kwenye utafiti huu ni watu walio kwenye ndoa itakayodumu kwa muda mrefu.

Hata hivyo mwanamke ataendelea kupanga uzazi hadi muda uliotengwa kufanya uchunguzi kwa mwanaume kuisha.
Mwanaume anayetarajia kufanya uzazi mpango sharti awe na umri wa kati ya miaka 18 hadi 50 huku mwanamke akiwa na umri wa 14 hadi 34.
Aina tofauti za uzazi wa mpango.
·        Kuweka Kitanzi
·        Kuweka kipandikizi/ Kijiti
·        Njia ya Vidonge
·        Njia ya sindano
·        Kutumia mipira ya kondom ya kike au ya kiume

Aina hizi huwa na madhara kwa akina mama kama vile;
Kupata ugumu wa kushika mimba baadaya ya matumizi ya muda mrefu,kuvunja damu mara kwa mara,kupungua au kuongezea kwa mwili na mabadiliko ya siku za hedhi.

Endapo ufanisi utapatikana kwenye jaribio hili basi itapunguza changamoto zinazowakabili wanawake katika shughuli zao za kuhakikisha wamepanga uzazi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni