Alhamisi, 13 Juni 2019

world blood donor day 2019



Kesho (June 14, 2019) ni siku ya maadhimisho ya utoaji damu duniani.

Image result for done la damu
Siku hii  ambayo huadhimishwa kila mwaka,imelenga kuwashukuru watu wote wanaojitokeza kutoa damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wagonjwa waliopungukiwa na damu na pia  walio kwenye  hatari ya kupoteza maisha kwa kukosa damu.
 Shirika la Afya duniani (WHO) na nchini wanachama wake zimelenga  kuwaelimisha watu   umuhimu wa kujitolea kutoa  damu mara kwa mara ili kuongeza paini za damu safi na salama kote duniani

Nchini Kenya kumekuwa na upungufu wa damu katika kituo cha Kitaifa cha kuhifadhi damu maana wakenya wengi hawapendi kutoa damu.

Mila,tamaduni na pia Imani za kidini zikichangia katika hali hii.

Serikali imekuwa katika harakati za kuwahamazisha wakenya umuhimu wa kutoa damu ilikuokoa maisha ya maelfu ya watu wanaokumbana na matatizo ya ukosefu wa damu ya kutosha mwilini.

Maadhimisho haya yatafanyika nchini Rwanda, maudhui yakiwa “damu salama kwa wote (safe blood for all).

Utoaji wa damu unasaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya watu kila mwaka kwani wagonjwa wanaougua na kuhatarisha maisha huokolewa na damu ambayo iko katika hifadhi au benki ya damu.

Wagonjwa wa dharula, wanaofanyiwa upasuaji wakiwemo wamama wanaotoka kujifungua ni miongoni mwa wale wanaonufaika na damu iliotolewa na watu kwa hiari.

Nchi nyingi zinakumbana na tatizo la upungufu wa damu katika benki za damu na tatizo la kupata damu safi na salama .
Ni jambo la muhimu watu kuelimishwa na kutambua mafanikio yanayotokana na kuchanga damu safi na salama.

Hatua hii itasaidia watu wengine walioko hospitalini wanaoteseka na tatizo la upungufu wa damu mwilini.

Shirika la kuhifadhi damu nchini Kenya (KNBTS),) inasema kuwa Kenya haijafikia viwango vya paini za damu iliyowekewa  na  shirika la Afya Duniani,kwa nchi wanachama wake.

Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), nchi inapaswa kuwa na paini 400,000 za damu kila wakati.

Hata hivyo,kiwango hiki kinaweza kufikiwa iwapo asilimia moja ya watu wangetoa damu mara moja kwa mwaka
sababu ikiwa  watu wengi hawapendi  kutoa damu na pia watu kukosa kuelewa umuhimu wa kutoa damu.
 Kwa muda mrefu  KNBTS imekuwa ikihamasisha Wakenya kujitokeza kutoa damu kupitia mitandao ya kijamii vyombo vya habari na mabango.
ajari za barabarani, mashambulizi ya kigaidi na kuongezeka kwa magonjwa yanayohitaji damu Zaidi yamechangia upungufu wa damu katika hifadhi.
Utoaji wa damu Kenya uko chini sana huku idadi ya wanaohitaji damu ikiongezeka kila siku.
Itakuwa changamoto kwa wakenya nan a watu wote kujitolea kutoa damu ili kuokoa maisha ya marafiki,wapendwa wetu n ahata watu tusiowafahamu.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni