(WHO photo) |
Shirika la afya duniani likishirikiana
na serikali ya Ufarasa imeweka mkataba wa pamoja kushirikiana katika harakati
zake za kuanzisha chuo cha mafunzo ya afya duniani huko Lyon,Ufaransa.
Makubaliano hayo yalifanywa na
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Gebreyesus na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko
Geneva,Uswizi.
Wabunifu watapata fursa kuonyesha ubunifu wao na kuchangia katika
mundo mbinu ya afya,katika harakati za kuinua viwango na huduma za afya duniani.
Kulingana na Shirika la Afya
Duniani(WHO)lengo la kufanya maazimiyo hayo na nia ya kuanzisha chuo cha mafunzo ya afya ni
kufanikisha shabaha ya WHO la kuhakikisha kuwa ifikiapo mwaka wa 2023 watu
billioni moja watafaidika kutokana na huduma bora za afya kote duniani.
Mafunzo yatatolewa na wataalamu wa afya
kulingana na kanuni na malengo ya shirika la afya duniani(WHO).
Viongozi,wasomi,watafiti ,wafanyi kazi
wa WHO, watu wote duniani waliohitimu watapewa nafasi ya masomo katika chuo
hiki.Ni sharti watoke nchi wanachama wa WHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni