Kenya imechukua hatua za dharula kuthibiti
ugonjwa wa ebola baada ya kijana mmoja kufariki huko Kasese ,Magharibi mwa Uganda
.

Watapimwa viwango vya joto mwilini.
Uganda ilitangaza kesi mbili za Ebola
baada ya kugunduliwa kwa kijana mwenye umri wa miaka mitano na virusi .
Duru
sinasem Mvulana huyo, alisema kuwa alisafiri pamoja na mama yake kutoka DRC
Jumapili, alifariki Jumanne usiku.
Kufuatia mlipuko wa Ebola shirika la
Afya Duniani likishirikiana na Serikali ya Uganda na mataifa jira inachukua
hatua za dharula kuhakikisha hali imethibitiwa.
WHO imesema
wahudumu wa afya 4700 wamepewa chanjo ya kuzuia maambukizi na wamejiandaa
kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
Dalili za ebola
·
Homa
·
Kufuja damu
·
Hutabulika baada ya siku ishirini na moja 21
·
Joto jingi
mwilini ya Zaidi ya kipimo cha 38 degree Homa
·
Kichefuchefu na kutapika
·
Kuharisha
·
Vidonda vya koo
·
Kuumwa kichwa
·
Maumivu ya misuli
·
Kusumbuliwa na tumbo
·
Kuchoka
·
Kukosa hamu ya chakula
Kinga
·
Osha mikono na sabuni: Jiepusha na tabia ya kutoosha mikono
·
Jiepushe na hali ya kumkaribia/kumguza
mtu aliyeabukizwa virusi vya Ebola
·
Epuka nyama ya pori
·
Epuka miili ya waliofariki kutakana na
maabukizi ya Ebola
Mwanzoni mwa Mwezi huu,shirika hilo la afya
ulimwenguni lilisema takriban watu 2,000 wameambukizwa ugonjwa huo nchini
Congo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni