Alhamisi, 27 Juni 2019

Trachoma


Trachoma (Vikope)

Trachoma au vikope ni ugonjwa unaosababisha upofu.isitoshe,maabukizi yake yanatokana na bakteria aina ya Klamidia Trakomati.

Ugonjwa huu unaweza kuthibitiwa ukitibiwa mapema.


Mazingira machafu na ukosefu wa maji safi huchangia maabukizi ya maradhi haya.

Nchini kenya jamii za wafungaji wa kuhamahama huadhrikika Zaidi.

Hata hivyo idadi ya magonjwa imepungua kwa asilimia 91 kote duniani

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya watu walio kwenye hatari ya maabuziki imepungua kutoka 1.5 billioni mwaka wa 2002 hadi 142 millioni mwaka  2019.

Tafiti zinaonyesha kuwa ,kati  ya nchi 44 ambazo ziko Afrika na Asia, zilikubwa na ugonjwa huu lakini umethibitiwa kwa kiwango cha juu kwa sasa.

WHO inasema kuwa, idadi ya waliohitaji upasuaji kurekebisha hali ya upofu ya trachoma imepungua kutoka millioni 7.6, mwaka  2002 hadi millioni 2.5 mwaka 2019.


Mbali na hayo,serikali ya Kenya imeweka mikakati ya kutokomeza tishio hili .

Mwaka wa 2015,Wizara ya Afya ilizidua mpango na miradi ili kuhakikisha Trachoma imekabiriwa mwaka 2019.


Mpango huu wa miaka mitano, ambao unatarajiwa kukamilika mwaka huu ulilenga kufanya upasuaji wa macho 40,000-katika maeneo yaliyo adhirika Zaidi. 

changamoto ya maambukizi


Kajiado,Samburu,isiolo,Laikipia,Baringo,Turkana,Meru Kaskazini ni baadhi ya maeneo 12 yaliotarajiwa kufaidika na mpango wa kukomesha Trachoma.

Watu Zaidi ya 2.9 millioni watapata matibabu, elimu ya afya ya umma kuhusu Trachoma,jinsi ya kujikinga, namna  yakudumisha usafi na mazingira masafi.

Hii ni hatua nzuri kwa serikali  kuhakikisha inatokomeza maambukizi mapya ya Trachoma kwa kuendelea kutoa dawa katika wilaya 12 zilizotajwa na kuwafanyia upasuaji wagonjwa ambao wamefikia hatua ya kupata upofu.

Serikali ya Kenya imekua ikishirikiana na serikali  Uingereza kupitia taasisi ya UK aid na Queen Elizabeth Diamond Jubilee Trust na shirika la Ugeremani la Christian Blind Mission katika kuhakikisha wagonjwa wa Vikope wanafikiwa na kupata huduma za matibabu pamoja na kufanyiwa upasuaji kwa wale ambao walio kwenye hatari ya  kupata upofu.


Majimbo ya Kajiado na Samburu yanaongoza kwa kiwango cha juu cha Trachoma.

Dalili
·         Macho kuwa mekundu.
·         Macho kutoa machozi kila wakati.
·         Maumivu na kuwasha macho.

Madhara

·         Kushindwa kustahimili mwanga na maumivu ya macho kwa watoto.

·         maamivu makali mgojwa anapopepesa macho kutokana na kuchomwa na vikope


·         kufifia uwezo wa kuona.

·         upofu kutokana na makovu kwenye kioo cha mbele ya jicho. 


·              Kinga

·         Kudumisha usafi wa mwili na mazingira ya makazi .


Matibabu
·         Matibabu ya mapema hupunguza vimelea vinavyoleta ugonjwa huu

·         Operesheni ndogo, kwa wagonjwa waliokwisha kupata vikope.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni