Jumanne, 5 Januari 2021

Oxford-AstraZeneca

 Chajo ya Oxford-AstraZeneca

Huku chanjo dhidi ya virusi ya Corona yaani COVID -19 ikianza kutolewa kwenye mataifa yalioendelea,kenya inatarajiwa kuanza kutoa chanjo hiyo mwanzoni mwa januari mwaka huu.

Hapo awali, Wizara Ya Afya ilitoa taarifa kuwa Shehena ya chanjo ya Covid-19 inatarajiwa nchini Kenya mwezi huu, huku walengwa wa kwanza wakiwa vikundi vilivyo katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi.

Isitoshe,Kenya imeagiza  dozi milioni 24 za chanjo ya Chuo Kikuu cha Oxford-AstraZeneca ambayo ni ya bei nafuu na inahifadhiwa kwa urahisi.

Baadhi ya walio kwenye hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona ni pamoja na Wafanyikazi wa afya, maafisa wa polisi, wazee na walimu .

Chanjo ya Chuo Kikuu cha Oxford-AstraZeneca itatolewa  katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

Kulingana na Wizara ya Afya watu ambao wanaokuwa kwenye mukushanyiko wa umati na wale walioadhirika na magonjwa mengine ya kiafya watakuwa wa kwanza kupewa chanjo dhidi ya coronavirus.

Inakadiriwa asilimia 20 ya idadi ya watu nchini watapokea chanjo katika awamu ya  kwanza.

Zaidi ya hayo, serikali inachunguza njia za kushirikiana na mashirika mengine kama yale ya Wachina ambayo yameunda vidonda vya Covid-19 na wengine.

Kwa sasa,Kwa sasa, Chanjo tatu ambazo zimefanyiwa utafiti dhidi ya COVID-19 ni ile ya Chuo kikuu cha Oxford inayojulikana kama AstraZeneca ,Pfizer’s kutoka kwa kampuni ya kutengeneza 

madawa na Moderna inayotolewa kwa matumizi ya dharula.

 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni