China yawazuia wataalam wa afya wa WHO
kuingia nchini humo.
Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO) limekemea
hatua ya Uchina,kuwazuia kuingia nchini humo kwa timu inayochunguza asili ya
janga la coronavirus.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dkt.Tedros
Adhanom Ghebreyesus alisema wanasayansi wawili wa timu ya Umoja wa Mataifa
tayari walikuwa wameondoka nchi zao kuelekea Wuhan, walipoambiwa kuwa maafisa
wa China hawajapitisha idhini zinazohitajika kuingia nchini.
Dkt.Ghebreyesus alisema alikuwa
akiwasiliana na Uchina kabla ya ziara ya wawili hao kuanza, na kila kitu
kilikuwa kamili baina yake na China.
Akihutubia wanahabari kutoka makao makuu ya
shirika hilo,huko geneva,uswizi,Dkt.Ghebreyesus alisema,"Nimesikitishwa
sana na habari hii."
"Nimekuwa nikiwasiliana na maafisa
wakuu wa China na nimeelezea kuwa ujumbe huu ni kipaumbele kwa WHO na timu ya
kimataifa."
azimio la kutaka uchunguzi huru.
Tedros alisisitiza kuwa madhumuni ya
mkutano huo ilikuwa kutaadhmini hali hilivyo kuwa na kiini cha mripuko wa coronavirusi,kama
ilivyopi asimiwa na mataifa mia moja ,mei mwaka uliopita.
Hapo awali, uchina ilikuwa imewahakikishia
kuwa ilikua kwenye harakati za kujiadaa kupokea ujumbe huo.
Maafisa wa WHO kwa muda mrefu wamekuwa
wakifanya mazungumzo na Beijing kuruhusu timu ya wanasayansi wake kupata fursa
kuchunguza asili ya virusi – vilivyo gunduliwa kwanza huko Wuhan mnamo Desemba
2019.
Katika mkutano na waandishi wa habari
Jumatano, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China, Hua Chunying, alisema Uchina
imekuwa na mtazamo wazi, uhuru na uwajibikaji kila wakati katika harakati za
kutafuta asili ya coronavirusi.
Hua alisema,hapo awali nchi yake,ilikuwa
imekaribisha wataalam wa WHO nchini na akasema kuwa timu ya uchunguzi ya Umoja
wa Mataifa na wataalam wa China wakuwa na ushirikiano wa mara kwa mara.
Alisema,ili kuhakikisha kuwa kikundi cha
wataalam wa kimataifa kinachokuja China kinaweza kufanya kazi vizuri,
inahitajika kutimiza taratibu zinazohitajika na kufanya mipango maalum
inayofaa.
Beijing imekuwa ikiishutumiwa jinsi
inavyochukulia swala hili hasa katika kuchunguza kiini za maambukizi ya virusi
vya COVID 19.
Hii imepelekea uhusiano wake na marekani
kuzorota.
Rais wa Merika Donald Trump amekuwa akilaumu
China mara kwa mara kwa kuregea kwake kukabili janga hili.
Kufuatia uhusiano mbaya kati ya nchi hizi
mbili,Marekani itasitisha uhusiano wake na WHO, ikisema kuwa Uchina haikuripoti
habari sahihi iliyokuwa nayo juu ya coronavirus na ilishinikiza WHO
"kupotosha ulimwengu."
Marekani imetaka uwazi katika shughuli za
WHO nchini China.
Pia inadaiwa kuwa maafisa wa China walitoa
habari za kupotosha kuhusu idadi ya kesi wakati wa hatua za mwanzo za mlipuko
wa Virusi ya Corona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni