kesho ni siku ya kimataifa ya hedhi duniani .
siku hii inaadhimishwa wakati kukiwa na changamoto chungu nzima hasa la ukosefu wa taulo za hedhi.Swala la hedhi linachukuliwa na jamii kuwa ni jambo ambalo halistahili kujadiliwa kwa uwazi.Pia tamaduni za kiafrika liliona kama ni mwiko kwa mwanamke aliyenahedhi kutangamana na wengine,na kuonekana kama mchafu.hivyo basi wasichana wanapovunja ungo wanaona haya kuzungumza na pia changamaoto jinzi ya kuzipata taulo.Wasichana wengi wanaostahili kuwa shuleni hupotesa muda mwingi nyumbani kila mwezi kutokana na hedhi.pia wanatumia njia ambazo sio salama kujizua wanapokuwa kwenye hedhi.Mashirika ya kijamii yamejitokeza kutoa pedi shuleni ilikuhakikisha wasichana hawakosi huhudhuria masomo,pia elimu kuhusu usafi na hedhi inatolewa. Unyanyapa au kutengwa wakati wa hedhi pia ni changamoto kwa wanafunzi wengi na ni muhimu kuelimisha jamii kuwa hili ni jambo la kawaida na halina aibu.
Wasichana wanapokosa hela ya kununua pedi,waohujihuzisha na maswala ya ngono za mapema ili wapate namna ya kupata pedi.swala hili huchangia ndoa za mapema. Suala la kupatikana kwa vifaa vya hedhi nalo limekuwa tatizo kutokana na bei yake kuwa juu lakini siku za karibuni baadhi ya nchi zimepitisha taulo za kike kuwa bure au kuondolewa kodi na ushuru kama njia ya kutokomeza umaskini utokanao na hedhi salama. Siku ya hedhi salama huadhimishwa tarehe 28 mwezi Mei kwa kuwa mzunguko wa hedhi kwa mwezi ni siku 28 na mtu anaweza kutokwa na hedhi kwa wastani wa siku 5 au 7 kila mwezi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni