Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2019

WHO -UHC (universal health Coverage)

Picha
Azimio la afya kwa wote Sekta ya afya duniani imepata mafanikio   mwafaka baada ya Viongozi wa ulimwengu kupitisha rasmi Azimio la Kisiasa la Umoja wa Mataifa kuhusu afya kwa wote   (UHC) ifikapo mwaka wa 2030. Kwenye kikao cha ngazi ya juu kuhusu afya kwa wote, katika Makao Makuu ya   Umoja wa Mataifa jijini New york, Marekani ,Viongozi walitoa hoja kuwa ni muhimu swala la afya kwa wote lishighulikiwe kwa haraka na wakaridhia lipitishwe rasmi na baraza kuu. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutumu kwenye kikao hicho alisema,ingawa afya ni haki ya kila mtu, bado nusu ya watu ulimwenguni   wanakosa haki yao ya msingi.   Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO amesema kuwa hii ni hatua muhimu na ni jukumu ya mataifa husika kuhakikisha malengo haya yameafikiwa ifikapo mwaka wa 2030. Dk Ghebreyesus akisema Ulimwengu umebakisha miaka 11 kuyatekeleza majukumu haya mwafaka ya afya. Aliwapongeza viongozi kwa kuchu...

chanjo ya malaria

Jaribio la chanjo ya malaria Huku ugonjwa wa malaria ukiwa miongoni mwa magonjwa hatari duniani,mbinu za kuukabili ugonjwa huu zinaendelea kuguduliwa kila uchao. Hii leo,nchi ya  Kenya itakuwa miongoni mwa nchi tatu barani Afrika zinazozindua majaribio ya chanjo ya kwanza ulimwenguni dhidi ya malaria. Nchi zingine kuzindua na kushiriki   katika mpango huu ni Ghana na Malawi. Zaidi ya watoto 300,000 chini ya miaka miwili wanatarajiwa kupewa chanjo hiyo kila mwaka Katika nchi zote tatu. Chanjo hiyo inayofahamika kama RTS,S ina mchanganyiko wa dawa inayoisaidia mfumo wa kinga mwilini kukabiliana na mbu wanaosababisha malaria. Hapo awali majaribio madogo yalionyesha kuwa karibu watoto wanne kati ya 10 kati ya umri wa miaka mitano na 17, waliopata dozi zote nne za chanjo hiyo, walilindwa. Chanjo hii imekuwa ikifanyiwa utafiti kwa zaidi ya miaka 30. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema hii inaweza kubadilika mchezo, lakini inasema chanjo hiyo in...