Jumanne, 24 Septemba 2019

WHO -UHC (universal health Coverage)


Azimio la afya kwa wote

Image result for universal health coverage new yorkSekta ya afya duniani imepata mafanikio  mwafaka baada ya Viongozi wa ulimwengu kupitisha rasmi Azimio la Kisiasa la Umoja wa Mataifa kuhusu afya kwa wote  (UHC) ifikapo mwaka wa 2030.
Kwenye kikao cha ngazi ya juu kuhusu afya kwa wote, katika Makao Makuu ya  Umoja wa Mataifa jijini New york, Marekani ,Viongozi walitoa hoja kuwa ni muhimu swala la afya kwa wote lishighulikiwe kwa haraka na wakaridhia lipitishwe rasmi na baraza kuu.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutumu kwenye kikao hicho alisema,ingawa afya ni haki ya kila mtu, bado nusu ya watu ulimwenguni  wanakosa haki yao ya msingi.

Image result for president kenyatta meets guterres in new york Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO amesema kuwa hii ni hatua muhimu na ni jukumu ya mataifa husika kuhakikisha malengo haya yameafikiwa ifikapo mwaka wa 2030.

Dk Ghebreyesus akisema Ulimwengu umebakisha miaka 11 kuyatekeleza majukumu haya mwafaka ya afya.

Aliwapongeza viongozi kwa kuchukua uamuzi wa kisiasa wa afya kwa wote.

Azimio hilo linakuja siku moja baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) na washirika wake kuweka mikakati ya kuboresha kwa mara mbili viwango vya afya  kabla ya mwaka 2030 ili kuhakikisha  watu bilioni 5 wasioweza kupata huduma ya afya hawaja achwa nyuma kwenye mpango huu.
Image result for rural kenya health facility
Hii ni  kuwa haya yakizingatiwa, hakuna mtu atapata ugumu wa kupata matibabu ya afya kwa kukosa pesa za kugharamia matibabu.

Pia serikali zinatarajiwa kutekeleza mipango ya kiafya yenye athari kubwa kupambana na magonjwa na kulinda afya ya wanawake na watoto.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Bill & Melinda Gates, Melinda Gates ambaye ni mfadhili mkuu kwenye sekta ya afya alisema huu ni wakati wa kufanya kazi kwa bidii ili  kubadili ahadi hizo kuwa matokeo.

Wafadhili na serikali za nchi zinahitaji kusonga mbele zaidi kama kawaida ili kusaidia mifumo ya huduma ya afya inayoshughulikia mahitaji mengi ya watu kwa maisha yao yote, "alisema Gates.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ni miongoni wa viongozi waliohudhuria kikao hiki.
Hapo awali,rais Kenyatta alikutana na Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Kenya ni mojawapo ya nchini inayofanya bidii kuhakikisha afya ya wote imepewa kibao mbele.

La muhimu ni kuhakikisha maswala ya afya yametekelezwa ili kupunguza idadi ya yaafa yanayokokea kutokana na ukosefu wa huduma za afya.

Mnamo tarehe 24 Septemba, WHO na mashirika mengine 11 ya kimataifa, ambayo kwa pamoja huchangia kwa  theluthi moja ya msaada wa maendeleo kwa afya, itazindua Mpango wao wa Global Action wa afya na ustawi kwa wote na kufikia malengo yanayohusiana na afya ya SDG.

Viongozi wa dunia  wataripoti juu ya maendeleo yao kwa Mkutano Mkuu wa U.N. mnamo 2023.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni