Jaribio la chanjo ya malaria
Huku ugonjwa wa malaria ukiwa miongoni mwa
magonjwa hatari duniani,mbinu za kuukabili ugonjwa huu zinaendelea kuguduliwa kila uchao.
Hii leo,nchi ya Kenya itakuwa miongoni mwa nchi tatu barani
Afrika zinazozindua majaribio ya chanjo ya kwanza ulimwenguni dhidi ya malaria.
Nchi zingine kuzindua na kushiriki katika mpango huu ni Ghana na Malawi.
Zaidi ya watoto 300,000 chini ya miaka miwili
wanatarajiwa kupewa chanjo hiyo kila mwaka Katika nchi zote tatu.
Chanjo hiyo inayofahamika kama RTS,S ina
mchanganyiko wa dawa inayoisaidia mfumo wa kinga mwilini kukabiliana na mbu
wanaosababisha malaria.
Chanjo hii imekuwa ikifanyiwa utafiti kwa
zaidi ya miaka 30.
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema hii
inaweza kubadilika mchezo, lakini inasema chanjo hiyo inatakiwa kutumika kwa
mbadala na viandarua na pia dawa .
Malaria inaua watu zaidi ya 400,000 kwa mwaka
- zaidi ya nusu yao wakiwa watoto kutoka
Afrika ,Jangwa la Sahara.
Waziri wa Afya wa Kenya Bi Cecily kariuki ataongoza
taifa kuzidua mpango huu katika jimbo la Homabay.Serikali imesema kuwa mpango
huo utajumuishwa katika mpango wa kitaifa wa chanjo.Huku watoto wa umri wa
miaka (6)sita,saba (7) na tisa (9)na miezi 24 wakipata chanjo
Majimbo ya
Kisumu,Migori,Bungoma,Busia,Siaya,Vihiga,Kakamenga na mombasa yatafaidika
katika mpango huu.
Ingawa serikali imechua hatua kukabili malaria
,bado changamoto ziko.
Hivi mrupuku wa malaria uliua watu wanane
Baringo.
Malaria huenezwa na kuumwa na mbu aina
ya Anofelesi.
Watoto wa umri wa chini ya miaka 5 wako katika
hatari zaidi ya kupata malaria.
Dalili
za Malaria
homa kali,
kuhara,
kutapika,
kuumwa kichwa,
Kutetemeka na kuumwa mwili mzima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni