Siku ya Kifua Kikuu Duniani
Siku ya Kifua Kikuu (TB) Duniani huamasishwa Machi 24kila
mwaka.lengo likiwa kufahamisha umma idadi ya maabukizi,vifo, juhudi za
kukomesha janga la TB na binu mpya zinazobuniwa ili kukabiliana na makali ya
ugonjwa wa TB. Mnamo Tarehe mwaka wa 1882 Dk Robert Koch alitangaza kwamba
amegundua bakteria inayosababisha TB, ambayo ilitoa fursa ya kutambua na
kuponya ugonjwa huu.
TB inasalia kuwa moja ya magonjwa hatari zaidi ya
kuambukiza ulimwenguni. Kila siku, zaidi ya watu 4100 hupoteza maisha kwa TB na
karibu watu 28,000 wanaugua ugonjwa huu unaozuilika na pia kutibika. Juhudi za
kimataifa za kukabiliana na TB zimeokoa maisha ya takriban milioni 66 tangu
mwaka wa 2000. Hata hivyo, janga la COVID-19 limerudisha nyuma maendeleo ya
miaka mingi iliyopatikana katika vita vya kukomesha TB. Kwa mara ya kwanza
katika zaidi ya muongo mmoja, vifo vya TB viliongezeka mwaka 2020.
Kauli mbiu ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani mwaka huu-2022,
ni ‘Wekeza Kukomesha Kifua Kikuu. Okoa Uhai.’ -inawasilisha hitaji la dharura
la kuwekeza rasilimali ili kuimarisha mapambano dhidi ya TB na kufikia ahadi za
kukomesha TB zinazotolewa na viongozi wa kimataifa. Hili ni muhimu hasa katika
muktadha wa janga la COVID-19 ambalo limeweka maendeleo ya kukomesha hatarini,
na kuhakikisha ufikiaji sawa wa kinga na matunzo kulingana na msukumo au kauli
ya Shirika La Afya Duniani( WHO)wa kufikia Huduma ya Afya kwa Wote.Uwekezaji
zaidi utaokoa maisha ya mamilioni ya watu zaidi, na kuongeza kasi ya kukomesha janga la TB.
Mwaka jana yaani
2021shirika la kimataifa la kufanikisha uwepo wa tiba nafuu duniani, UNITAID
linaloratibiwa na shirika la afya afya dunianui, WHO,lilizidua dawa mpya ya kukabiliana na TB aina ya Rifapentine
ambayo tayari imeanza kutolewa na kutumiwa katika nchi tano zenye kiwango
kikubwa zaidi cha TB barani Afrika .nchi hizo ni Ethiopia, Ghana, Kenya,
Zimbabwe na Msumbiji. Wakati wa uziduzi huo, mjini Geneva, Uswsi , Msemaji
wa UNITAID Herve Verhoosel akizungumza na waandishi wa habari alisema “UNITAID
alisema kuwa tiba hiyo mpya ni ya
gharama nafuu. Tiba mpya gharama yake ni nafuu kwa asilimia 70 kuliko dawa
zaa wali. Inaitwa Rifapentine na kwa majadiliano kati ya UNITAID na wadau wake,
dawa hii inaweza kupatikana katika nchi zaidi ya 100 kwa gharama ya dola 15
badala ya dola 45.”
WHO ilipendekeza
matumizi ya tiba hii mpya kwa watu wagonjwa wa Kifua Kikuu kilichofikichika
ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi, VVU na wagonjwa wengine wenye Kifua Kikuu na
wa umri wowote. Utafiti umebaini kuwa wagonjwa wana uwezo mkubwa wa kukamilisha
matibabu katika kipindi kifupi. Wagonjwa wa Kifua Kikuu wanaweza
kuambukiza ugonjwa huo kwa watu kati ya 10 hadi 15 wanaokaribiana nao kwa mwaka
mzima ambapo UNITAID inasema bila tiba sahihi, asilimia 45 ya watu wasio na VVU
wenye Kifua Kikuu na watu wenye VVU na Kifua Kikuu wanaweza kufariki
dunia.
licha ya
Kifua Kikuu kuwa ugonjwa unaozuilika na kutibika, bado ni moja ya magonjwa
hatari zaidi ya kuambukiza ukisababisha vifo vya watu milioni 1.5 kila mwaka
wakiwemo watu 250,000 wanaoishi na virusi vya Ukimwi.”
Maambukizi ya TB
Inakadiriwa
kuwa mwaka 2019, watu wapatao milioni 10 waliambukizwa Kifua Kikuu, idadi
ambayo imekuwa ikipungua taratibu mno katika miaka ya karibuni. Katika idadi
hiyo milioni 5.7 ni wanaume, milioni 3.2 wanawake na milioni 1.1 ni watoto na
idadi kubwa wanaishi katika nchi za kipato cha chini na kati. Kitaifa,
nchi zenye wagonjwa zaidi wa Kifua Kikuu ni India, Indonesia, China,
Ufilipino, Pakistani, Nigeria, Bangladesh na Afrika Kusini.
Tangu kuibuka
kwa Janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 wagonjwa wa TB wamepata
changamoto kupata matibabu.Covid-19 limekuwa mwiba katika tiba dhidi ya kifua
kikuu kwa kuwa linavuruga utoaji wa huduma za Kifua Kikuu.
Baadhi ya dalili
za ugonjwa wa Kifua Kikuu ni kama vile;homa, kupungua uzito, maumivu ya miguu,
kukosahamu ya chakula na kukohoa kwa muda mrefu.