saratani ya matiti
Saratani haina huruma Huku mwezi wa kumi ukiwa mwezi wa kupambana na ugonjwa wa saratani,ugonjwa huu unaendelea kuwa tishio kwa wengi.Kwa muda wa chini ya mwezi mmoja sasa,Kenya na pia ulimwengu kwa ujumla imepoteza watu mashuhuri kutokana na Saratani. Mwenda zake Mama Wangari Maathai, ammbaye atakumbukwa kwa kulinda na kuhifadhi mazingira. Mwanzilishi wa kampuni ya Apple Steve Jobs ambaye aligobe katika nyanja ya technologia ya habari(alibuni mitandao) Mwingine ni Dkt Margaret Ogolla ,mtaalam wa afya ya watoto. Wa karibuni kufa saratani ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa ,Moijo Ole Keiwua aliyefariki siku moja tuu baada ya maziko ya Prof. Wangari Maathai. Saratani haichangui wala kubagua Kila mwezi wa Kumi, kampeni za mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani inafanyika.Kila kituo cha afya na pia watalaamu wa afya wanakuwa kwenye mstari wa mbele kuendeleza elimu na matiba.Hospitali ya Aga Khan ina kitengo maalum cha ugonjwa wa saratani.Pia uchunguzi wa saratani u...