Saratani haina huruma
Huku mwezi wa kumi ukiwa mwezi wa kupambana na ugonjwa wa saratani,ugonjwa huu unaendelea kuwa tishio kwa wengi.Kwa muda wa chini ya mwezi mmoja sasa,Kenya na pia ulimwengu kwa ujumla imepoteza watu mashuhuri kutokana na Saratani.
Mwenda zake Mama Wangari Maathai, ammbaye atakumbukwa kwa kulinda na kuhifadhi mazingira.
Mwanzilishi wa kampuni ya Apple Steve Jobs ambaye aligobe katika nyanja ya technologia ya habari(alibuni mitandao)
Mwingine ni Dkt Margaret Ogolla ,mtaalam wa afya ya watoto.
Wa karibuni kufa saratani ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa ,Moijo Ole Keiwua aliyefariki siku moja tuu baada ya maziko ya Prof. Wangari Maathai.
Saratani haichangui wala kubagua
Kila mwezi wa Kumi, kampeni za mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani inafanyika.Kila kituo cha afya na pia watalaamu wa afya wanakuwa kwenye mstari wa mbele kuendeleza elimu na matiba.Hospitali ya Aga Khan ina kitengo maalum cha ugonjwa wa saratani.Pia uchunguzi wa saratani unatolewa bila malipo.
Hii ni changa moto kwa serikali pia kufuata mwelekeo huu ilikukabiliana na ugonjwa huu mapema.
Lakini la kushangasha ni jinsi kampeni dhidi ya saratani hasusan ya matiti inavyoelekezwa zaidi kwa wanawake.
Wanaume wamebaguliwa wamekuwa hawana wa kuwanenea.
Katika kampeni zinazoendelezwa hapa nchini Kenya , wanawake wamepewa kipao mbele.
La kuhuzunisha na hakika ni kuwa, wanaume pia wapo hatarini ya kuabukishwa saratani ya matiti.saratani hii haibagui wala haichagui.wanaume kwa wanawake wako hatarini.
Hivyo basi ni jukumu la wataalamu wa afya kuwashirikisha au kuwahuzisha wote kwenye kampeni zao.
Serikali pia inajukumu hilo hilo .
Inaaminika kuwa saratani ya matiti inapomwaadhiri mwanamume anakuwa hatarini zaidi,endapo haitagunduliwa mapema kwani inaenea zaidi kwenye mbavu na sehemu nyingine za mwilini kuliko ile ya mwanamke.
Zaidi ya hayo ni jukumu pia ya wanaume kuhakikisha kuchunguza afya zao mara kwa mara, ili endapo mtu atapatikana na ugonjwa huu ajitibishe mapema.Kugunduliwa na kuendelea na tiba kama ile ya chemotherapy ni muhimu.Pia kuna matumaini ya kupona jambo ambalo ni kinyume ikiwa saratani itagunduliwa ikiwa imeenea mwilini.
Dalili
♦Kuwepo kwa uvimbe kwenye sehemu za kwapa
♦Sehemu ya titi kuingia ndani
♦Mabadiliko kwenye chuchu,
♦kidonda kwenye chuchu
♦chuchu hutokwa damu au maji yasiyo ya kawaida
♦ngozi kuwa na rangi nyekundu,
Vipimo vya Saratani ya Matiti
Utafiti unaonyesha Kuna kuna vipimo ambavyo hufanywa na wataalamu wa afya kubainisha kuwa mtu ana au hana saratani ya matiti.
X-ray ya matiti au Mammogram ambayo inaonyesha ikiwa kuna uvimbe au vivimbe kwenye matiti
Ultra-Sonography ni kipimo kinachosaidia kutambua iwapo uvimbe uliopo ndani ya matiti au titi umejaa maji ama hauna ili ufanyiwe vipimo zaidi.
Fine Needle Aspiration and Cytology (FNAC) Hii ni aina ya Kipimo kinachofanywa kwa kuchukua sehemu ya uvimbe (Aspiration) kwa kutumia aina fulani ya sindano (fine needle) na kisha kupeleka maabara sehemu iliyochukuliwa kwa ajili ya kutafitiwa zaidi ili kugundua uwepo wa saratani.
Surgical biopsy huu ni upasuaji mdogo unaofanywa kwenye titi lililoathirika kwa ajili ya kuchukua sehemu ya titi na baadaye kuipeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Sentinal lymph node biopsy – Hapa mgonjwa anapimwa ili kujua kama saratani imesambaa hadi kwenye tezi.
PET Scan hiki ni kipimo cha aina yake ambacho bado hakijafika au ni adimu katika nchi zinazoendelea. MRI na PET sinapatikana ncini Kenya
Tiba ya saratani ya matiti
Upasuaji
Sababu kuu ya upasuaji ni kuondoa saratani kwenye titi pamoja na tezi (lymph nodes). Kuna aina kadhaa za upasuaji unaoweza kufanywa kwenye titi lililogundulika kuwa na saratani.
Aina hizo ni pamoja na
Lumpectomy: Upasuaji huu hufanywa kuondoa sehemu ya saratani pamoja na sehemu ya titi ambayo haijaathirika kwa saratani. Baadaye i hufuatiwa na tiba ya mionzi (radiotherapy) kwa muda wa kati ya wiki 6 hivi.Mgonjwa anayepata tiba hii hupata uwezekano wa kuishi muda mrefu.
Simple ama Total mastectomy: Ni aina ya upasuaji inayohusisha uondoaji wa titi lote lililoathirika na saratani
Radical mastectomy:Aina hii ya upasuaji uhusisha uondoaji wa titi lote na kundi la tezi liloathirika kwa saratani, pamoja na misuli ya sehemu za kifua (chest wall muscles). Zaidi ya hayo , upasuaji wa aina hii hautumiki sana .
Modified radical mastectomy: Huu ni uondoaji wa titi lote lililoathirika pamoja na kundi lote la tezi (lymph nodes) chini ya mkono ila tu misuli ya kifua haiondolewi.
Tiba ya saratani kwa njia ya dawa (Systemic therapy)
Kulingana na wataalam wa afya, tiba ya aina hii inahusisha matumizi ya kemikali maalum za kutibu saratani (chemotherapy) pamoja na matumizi ya homoni (hormonal therapy).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni