Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2012

Kifua kikuu (TB)

Picha
Hatua za Kenya Kenya imepiga   hatua madhubuti   katika juhudi zake za kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Kenya imeorodheswa 15 kwenye orodha ya nchi 22 ambazo ugonjwa wa kifua kikuu ungali ni tishio. Zaidi ya hayo, Shirika la Afya Duniani linaarifu kuwa juhudi za pamoja zimesaidia kupunguza vifo kwa asilimia 40 tangu mwaka 1990.   Watu milioni 46 wameponywa kuanzia mwaka 1995 kutokana na juhudi za Umoja wa Mataifa, serikali mbalimbali, wafadhili, makundi ya kijamii, washirika binafsi, wataalamu wa afya, na makumi ya maelfu ya watumishi wa idara za afya pamoja na familia na jumuiya zilizoathirika Umaskini na Virusi vya ukimwi unachangia pakubwa   katika maambukizi ya   kifua kikuu katika nchi zinazoendelea. Kwa kawaida, wagonjwa ambao wanapatikana na magonjwa ya kuambukiza mara kwa mara hutengwa kuzuia kueneza ugonjwa.Hii hufanyika katika wodi maalum katika hospitali za serikali. Mkurugenzi wa maradhi ya ki...