Alhamisi, 29 Machi 2012

Kifua kikuu (TB)





Hatua za Kenya

Kenya imepiga  hatua madhubuti  katika juhudi zake za kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Kenya imeorodheswa 15 kwenye orodha ya nchi 22 ambazo ugonjwa wa kifua kikuu ungali ni tishio.

Zaidi ya hayo, Shirika la Afya Duniani linaarifu kuwa juhudi za pamoja zimesaidia kupunguza vifo kwa asilimia 40 tangu mwaka 1990.

 Watu milioni 46 wameponywa kuanzia mwaka 1995 kutokana na juhudi za Umoja wa Mataifa, serikali mbalimbali, wafadhili, makundi ya kijamii, washirika binafsi, wataalamu wa afya, na makumi ya maelfu ya watumishi wa idara za afya pamoja na familia na jumuiya zilizoathirika

Umaskini na Virusi vya ukimwi unachangia pakubwa  katika maambukizi ya  kifua kikuu katika nchi zinazoendelea.

Kwa kawaida, wagonjwa ambao wanapatikana na magonjwa ya kuambukiza mara kwa mara hutengwa kuzuia kueneza ugonjwa.Hii hufanyika katika wodi maalum katika hospitali za serikali.

Mkurugenzi wa maradhi ya kifua kikuu katika Wizara ya Afya ,Kenya Dkt. Joseph sitienei anasema orodha hii ni wazi kuwa Kenya imepiga hatua ya haraka ya kuhakikisha kuwa ugonjwa wa kifua kikuu umedhibitiwa.

Mwaka jana wagonjwa wawili wa kifua kikuu walitiwa baloni kwa madai kuwa walikata kumeza tembe zao kama walivyo agizwa na watalaamu wa afya.

Ingawa hatua ya selikali ilikemewa na wadau wa haki za binadamu, serikali ilichukua hatua kali dhidi ya wawili hao, kwa lengo la kuokoa maisha yao.

Kutozingatia maagizo ya daktari au kukosa tiba ya ugonjwa huu, ni hatari kwa maisha ya mwenye maradhi haya.

Mwishoni mwa mwaka 2009 Kenya ilikuwa na wagonjwa 110,065 wa TB.

Mwaka 2009, Kenya ilikuwa na matukio 500 ya TB sugu kwa madawa mengi ijulikanayo kama MDR-TB, idadi ambayo imeshuka hadi 334 mwaka huu.

Ni wagonjwa 117 tu waliotumia tiba.Idadi hii imepungua hadi 101 kote nchini.

Kulingana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki – Moon, Mnamo mwaka 2010 pekee, takriban watu milioni tisa waliambukizwa  maradhi ya kifua kikuu, ambapo watu 1.4 miongoni mwao walifariki, huku asilimia 95 ya vifo vikitokea katika nchi zinazoendelea.


Moon ametoa wito kuwepo kwa mshikamano wa kimataifa utakaohakikisha watu wote wakohuru dhidi ya hofu kuambukizwa kifua kikuu.alisema kuna haja ya kukomesha upuuzaji na kutilia maanani juhudi za kupunguza vifo zaidi.

 MDR-TB ni sugu kwa madawa mengi ya mstari wa kwanza. Hata hivyo, inaweza kutibiwa kwa kutumia tiba ya muda mrefu yenye gharama kubwa ya madawa ya mstari wa pili, ambayo yana madhara zaidi.

Kumtibu mgonjwa mmoja kuhitaji madawa yenye thamani ya zaidi ya dola 16,250.


Kifua kikuu ni ugonjwa ambukizi nambari mbili kwa mauaji ulimwenguni.


 
kifua kikuu



Kifua Kikuu (TB) ni ugonjwa ambao kwa kawaida huathiri mapafu. Kifua Kikuu wakati mwingine huathiri sehemu nyengine za mwili, kama vile ubongo, figo, au uti wa mgongo. Ugonjwa wa Kifua Kikuu unaweza kusababisha kifo usipotibiwa.

Viini vya Kifua Kikuu husambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia hewa. Viini vya Kifua Kikuu huwekwa hewani wakati mtu aliye na ugonjwa wa Kifua Kikuu anakohoa, kupiga chafya, kucheka, au kuimba. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni