Mpango mpya kuboresha huduma za uzazi wa kupanga baada ya kujifungua mimba: WHO
Unyonyeshaji mtoto baada ya kujifungua ni mojawapo ya njia za uzazi wa mpango- WHO
Shirika la Afya Duniani, WHO, limezindua mpango mpya wa
kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa kupanga kwa akina mama
katika miezi 12 ya kwanza baada ya kujifungua, ambao unawalenga wahudumu
wa afya na watunga sera. Kwa mujibu wa WHO, mimba zinazokaribiana sana
au zisizotarajiwa ni tishio la kiafya kwa mama na mtoto, na kwamba
kuweka pengo la angaa miaka miwili kabla ya mimba nyingine kunaweza
kuepusha asilimia 10 ya vifo vya utotoni na takriban kuepusha kifo
kimoja kati ya vitano miongoni mwa watoto wenye umri kati ya mwaka mmoja
hadi minne. Mpango huo ambao umezinduliwa katika kongamano la kimataifa
kuhusu uzazi wa kupanga mjini Addis Ababa, Ethiopia, unanuia kuitikia
mahitaji kwa ngazi zote za huduma za afya, ili kuongeza upatikanaji wa
huduma za uzazi wa mpango kwa akina mama mara tu baada ya kujifungua.
Takwimu kutoka nchi 27 zinazoendelea zinaonyesha kuwa asilimia 95 ya
wanawake wanataka kujiepusha na mimba kwa angaa miaka miwili baada ya
kujifungua, lakini asilimia 65 kati yao-Redio ya UM
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni