Habari njema ni Kwamba wanaougua fistula sasa wana sababu ya kutabasamu.
Hospitality kuu ya kitaifa ya Kenyatta kwa ushirikiano na wadau wengine katika sekta ya afya wametangaza kuwa kuanzia tarehe 4-18 Julai mwaka Huu watatoa matibabu ya bure kwa wote.
Huduma hii inatolewa bila malipo ilikumrudishia hadhi mwanamke anaye baguliwa, kukejeliwa na kuteswa na jamii kufuatia Hali yake.
Baadhi ya akinaHabari mama ambao wamefaidika kupitia Huduma hii wanasema wamezaliwa upya na wanasababu ya kuishi tena.
Kuna wengine ambao wamejiua kufuatia unyanyapa na kutekelezwa na jamii.
je fistula ni nini?
Tundu kwenye mango was uzazi. Tundu hili linaweza kutokea kati ya uke na njia ya haja kubwa au kati ya kibofu na uke baada ya mama kushindwa kujifungua au kutumia muda mrefu kujifungua. Pia kunajisiwa kunaweza kusababisha hali hii.Matokeo yake ni kwamba wanawake wenye fistula hujikuta katika matatizo makubwa ya kutokwa ovyo na mkojo au na kinyesi.Mara kwa mara wao hutengwa na jamii na kudharauriwa.Mwishowe wengi hujitia kitanzi kwa sababu ya machungu.
Kenya ni nchi ambazo zimepiga hatua kuhakikisha angalau akina mama na wakenya wa jumla wamehamasishwa kuhusu madhara yake ya namna ya kukakabili hali hii.kulingana na takwimu za UNFPA zaidi ya visa 3,000 hulipotiwa kila mwaka huku.Kuna hospitali chache hapa nchini ambazo zinafanya upasuaji wa kurekebisha hali hii, kamaHospitali kuu ya Kenyatta na Moi referal,Eldoret.
Hata hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa wakenya wamepata mafunzo kuhusu afya ya uzazi ili wajue kuna tiba ya fistula.Hali ya wasichana wadogo kukumbwa sana na fistula ya uzazi inahusishwa kwa karibu zaidi na kutokomaa vizuri kwa miili yao na nyonga zao.
Mara nyingi fistula ya uzazi huwakumba watu wanaoishi maeneo ya vijijini ambako kuna uhaba mkubwa sana wa watoa huduma wenye ujuzi.zaidi ya hayo,baadhi ya watu niliowahoji hawajui kuna tiba ya fistula hasa vijini.Wengine hawajui aina za mpango wa uzazi walio chini ya miaka kumi na nane na ushirini.
ukosefu wa ushauri kwa hakika kunachangia wasichana wengi kujikuta katika haliMwaka wa 1992 na 2001 upazuaji kerekebisha hali hii uliongezeka kutoka 36 hasi 479 kwa mwaka.Hatua ya kujia moyo ingawa mengi yahitajika.Huenda hali hii ya akina mama wawili wanaoadhirika wakijifungua kati ya akina mama 1,000 ikaimarika katika siku za karibuni.Tuna watakia akina mama wanaojifungua baraka zake maulana
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni