Tuna uwezo wa kudhibiti saratani: WHO
Tunapo adhimisha siku ya saratani,ugonjwa huu enaenea kwa kasi,lakini jambo la kufurahisha ni kuwa unaweza kudhibitiwa.
Maadhimisho ya mwaka huu yanaangazia mbinu zinazotumiwa na shirika la afya ulimwenguni, WHO kupunguza mzigo wa ugonjwa huo unaosababisha vifo vya watu Milioni Nane duniani kote kila mwaka.
WHO inasema kuna nyendo thabiti duniani zinazochochea ongezeko la visa vya saratani hususan kwenye nchi za vipato vya kati na chini ikiwemo uzee, ukuaji holela wa miji na mifumo ya maisha isiyo ya kiafya.
Hata hivyo WHO kupitia ujumbe wa mwaka huu Hauzidi uwezo wetu, inasema jitihada za pamoja zinaweza kudhibiti kitisho hicho kama anavyosema Nelly Enwerem-Bromsom wa mpango wa matibabu ya saratani kutoka shirika la nishati ya atomiki duniani, IAEA.
Bromsom anadokesa kuwa kuna haja kama jamii ya kimataifa kama jamii ya kimataifa kuungana kupitia teknolojia bunifu, uchangiaji wa fedha na kushirikiana kukabili mzigo wa ugonjwa huu wa saratani,unaoua zaidi ya wagonjwa Milioni Tano kila mwaka kwenye nchi zinazoendelea. Idadi hii ni zaidi ya wale wanaofariki dunia kwa Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni