Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2015

polio(ugonjwa wa kupooza)

Picha
Ugonjwa wa kupooza Polio ni ugonjwa unaopooza viungo endapo mtoto hatapata chanjo .Vifo pia hutokea. Kulingana na kauli ya mashirika ya afya na hasa lile la Afya Duninani (WHO)ni haki ya kila mtoto kupata matibabu yafaayo.Chanjo ya polio ikiwa mojawapo. Kutofanya hivyo basi kunachukuliwa kama kuvunja sheria na hatua za kiseria zinaweza kuchukuliwa kwa yeyote.   Hata hivyo,nchini Kenya kumekuwa na utata kuhusu uharisi wa chanjo hii ya polio. Wataalamu wa afya wanaokutoa ushauri kwa kanisa katoliki wameonya kuwa chanjo hii inachemikali ambazo zinaweza kudhuru afya ya uzazi kwa watoto hao baadaye. Daktari Stephen Karanja anayewakilisha kanisa katoliki anasema kuwa aliwasiliana na wizara ya afya nchini ,lakini maoni au malalamiko yao hayakushughulikiwa. Anasema kuwa   walifanya utafiti na kugundua kuwa kuna madini ambayo ina madhara ya   baadaye.Watoto hawa wataadhirika kwenye viungo vyao vya kizazi na hivyo kuwa vigumu kupata uzazi. |”maradhar...

Colposcope

Picha
Kifaa cha tiba Saratani ya shingo ya uzazi Katika shughuli za kila siku ubunifu na utumiaji wa teknologia za kisasa ni masawala yanayobatana,hasa katika sekta ya afya.   Ni hakika   kuwa ugonjwa au maradhi tofauti kugunduliwa mwilini mwa mwanadamu au wanyama na viumbe vingine , technogojia sharti itumiwe. Kufuatia ongezeko la idadi ya wanaougua ugonjwa wa saratani,watafiti wa afya wamebuni mbinu kabambe   za   kukabiliana na ugonjwa huu. Watafiti wawili kutoka   Israeli,Ariel Beery na David levitz wameunda kifaa ambacho kina uwezo wakugundua   saratani ya shingo ya uzazi . Kifaa hiki kinatumia simu ya mkononi na matokeo yake ni kamili na yanayotokea papo hapo.Hii ikiwa nafasi mwafaka ya kuanzisha matibabu ya mara moja. Muuguzi anatumia simu kunasa picha kwenye sehemu ya uzazi na kuhifadhi matokeo ya moja kwa moja. Kifaa hiki kijulikanacho kama Colposcope kimefanyiwa jaribio nchini Kenya mwezi julai katika kongamano la ...