Alhamisi, 13 Agosti 2015

polio(ugonjwa wa kupooza)


Ugonjwa wa kupooza

Polio ni ugonjwa unaopooza viungo endapo mtoto hatapata chanjo .Vifo pia hutokea.

Kulingana na kauli ya mashirika ya afya na hasa lile la Afya Duninani (WHO)ni haki ya kila mtoto kupata matibabu yafaayo.Chanjo ya polio ikiwa mojawapo.

Kutofanya hivyo basi kunachukuliwa kama kuvunja sheria na hatua za kiseria zinaweza kuchukuliwa kwa yeyote.
Image result for polio vaccine 
Hata hivyo,nchini Kenya kumekuwa na utata kuhusu uharisi wa chanjo hii ya polio.
Wataalamu wa afya wanaokutoa ushauri kwa kanisa katoliki wameonya kuwa chanjo hii inachemikali ambazo zinaweza kudhuru afya ya uzazi kwa watoto hao baadaye.

Daktari Stephen Karanja anayewakilisha kanisa katoliki anasema kuwa aliwasiliana na wizara ya afya nchini ,lakini maoni au malalamiko yao hayakushughulikiwa.

Anasema kuwa  walifanya utafiti na kugundua kuwa kuna madini ambayo ina madhara ya  baadaye.Watoto hawa wataadhirika kwenye viungo vyao vya kizazi na hivyo kuwa vigumu kupata uzazi.
|”maradhara haya yataonekana baada ya miaka kumi na tano” asema daktari Karanja.

Lakini kwa upande wake,serikali inapinga madai haya nakusisitisha kuwa hakuna haja ya kutoa tisho kwa wananchi,”hii chanjo haina madhara yeyote huu ni uvumi tu”,matamshi yake mkurugenzi wa huduma za afya Kenya,Dkt Nicholas Muraguri.

Anasema kuwa chanjo hiyo haina homoni ambayo inaadhiri afya ya uzazi.
Chanjo hii inatolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na shirika la watoto na elimu duniani(UNICEF) imepokea tetesi sawa huko Nigeria hapo awali.

Mwaka 2003,viongozi wa kanisa na wale wa siasa walitangaza kuwa chanjo ya polio ilikuwa ni tishio kwa maisha ya watoto huko kano,zamfara na kaduna kaskazini mwa nchi ya Nigeria.

Kufuatia wito kususia chanjo ,mkurupuko wa polio uliripotiwa na maafa zaidi ya 600 katika nchi hiyo na maabukizi kwenye nchi jirani.

Image result for dr stephenkaranja on polio
Dkt Karanja,,gaenokologia
Wakati tetesi kama hizo zinapoibuka wananchi huwa na hasira na wanaotoa huduma hiyo.visa vya masabulizi yameripotiwa katika vituo tofauti nchini na pia afrika kwa jumla.

Zaidi ya hayo,mwaka 2013,huko Nigeria, wauguzi tisa waliokuwa wakitoa chanjo waliuawa huko Kano.

Wapiganapo nyati wawili nyasi ndiyo huumia.Imekuwa ni futa ni kufute kati ya serikali na kanisa  huku wakuumia wakiwa ni watoto ambayo hawajui ukweli uliko.

Waumini wa kanisa katoliki  wamekataa kupeleka watoto wao kwa chanjo hiyo wakiwa na imani kuwa kanisa linayoyasema ni ukweli mtupu.

Nilifanya mahojiano na baadhi ya akina mama wakikatoliki ambayo wanasema kuwa wanaimani chanjo ya polio ina kasoro kwani kanisa haliwesi kuwatakia mambaya.

Huku baadhi wa wananchi wakisusia chanjo wengine waloinekana kuwapeleka watoto wao bila kujali kuwa kwa kweli kuna kasoro kwenye chanjo hii au ni uvumi tu.

Endapo kanisa ina uhakika kunashida,ukweil ni kwamba itachukua miaka kumi na tano na zaidi kujia ni nani anasema ukweli.

Lakini wadadisi wanasema uamuzi wa kanisa kususia chanjo ni hatati kwani kanisa katoliki hapa nchini Kenya ni baadhi ya mashirika yayongoza katika sekta ya afya.
Ni kwa sababu hii kanisa haliwezi kupuuzwa katika maswala ya afya.

Kanisa katoliki linamiliki hosptali 58,vituo vya afya 83,zahanati 311 na vituo vya kutoa masomo ya afya 17 nchini Kenya.

Serikali pia kupitia mkurugenzi wa afya wanasisitiza kuwa shughuli hiyo ilikuwa na mafanikio,na waliweza kutoa chanjo kwa kiwango walicho tarajia.


Itakuwa ni jambo la busara kwa kanisa na serikali kukaa kwa meza ya majadiliano na kupata suluhu ya dharula ili kuepusha maafa au kupooza kwa watoto wasiokuwa na hatia




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni