homa ya mapafu(Pneumonia)
Pneumonia Homa ya mapavu ni ugonjwa ambao unaathiri mapafu na unaua watoto kwa wingi hasa katika nchi zinazoendelea duniani. Ugonjwa wa nimonia umetajwa kuwa ugonjwa hatari na unauwa kwa kasi sana,huku idadi ya maafa yakiongezeka kila siku. nchini Kenya. Ripoti ya wizara ya afya ,Kenya inasema kuwa idadi ya wanaofariki imeongezeka maradufu. Pia watoto wameathirika Zaidi,inakadiriwa kwamba watu karibu 21,640 walifariki mwaka wa 2013 huku idadi ikiongezeka hadi 22,473 mwaka uliopita wa 2015. Hii ni changamoto kwa sekta ya afya kwani kuna mbinu za kupunguza makali ya nimonia. vifo hivi vinavyotokana na homa ya mapafu(nimonia) ,vinaripotiwa wakati madaktari na wauguzi wamekuwa wakifanya migomo kulalamikia mishahara duni na pia mazingira mabaya ya kufanyia kazi. Hii ni jambo ambalo si la kuchangamkiwa ,na ni sharti wizara ya afya itekeleze majikumu yake ipasavyo. Ni husuni kusuhudia maafa ya kila mara ,hasa kwa waz...