Pneumonia
Homa ya mapavu ni ugonjwa ambao unaathiri mapafu na unaua watoto kwa wingi hasa katika nchi zinazoendelea duniani.
Ripoti ya wizara ya afya ,Kenya inasema kuwa idadi ya wanaofariki imeongezeka maradufu.
Pia watoto wameathirika Zaidi,inakadiriwa kwamba watu karibu 21,640 walifariki mwaka wa 2013 huku idadi ikiongezeka hadi 22,473 mwaka uliopita wa 2015.
Hii ni changamoto kwa sekta ya afya kwani kuna mbinu za kupunguza makali ya nimonia.
vifo hivi vinavyotokana na homa ya mapafu(nimonia) ,vinaripotiwa wakati madaktari na wauguzi wamekuwa wakifanya migomo kulalamikia mishahara duni na pia mazingira mabaya ya kufanyia kazi.
Hii ni jambo ambalo si la kuchangamkiwa ,na ni sharti wizara ya afya itekeleze majikumu yake ipasavyo.
Ni husuni kusuhudia maafa ya kila mara ,hasa kwa wazazi katika sehemu za majimbo ambako hali ni mbaya Zaidi.
mwezi uliopita,jimbo la Nakuru lilikuwa na idadi kuwa ya maabukuzi na maafa ya ugonjwa huu.
kwenye kaunti ya Nakuru , watoto takriban 20 waliaga
dunia kutokana na ugonjwa wa Pneumonia katika kipindi cha mwezi mmoja.
Waziri wa afya kwenye kaunti
hiyo Mungai Kabii alisema kesi zingine 117 ziripotiwa kwenye vituo vya afya
kadhaa kwenye eneo hilo na pia kwenye kaunti zingine jirani.
Kufuatia mkurupuko huu, sampuli ya damu kutoka kwa walioathiriwa
zimetumwa kwenye maabara za shirika la KEMRI ili zifanyiwe utafiti huku wauguzi
wakitafuta namna na mbinu za kuudhibiti,
Alisema watoto wenye umri wa kati ya siku moja na miezi kumi na moja
ndio wako katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa.
Dalili za nimonia
Joto
kupanda, kutokwa na jasho unyonge wa mwili pamoja na kukohoa,homa,kuhisi baridi,kutoa sauti isiyo ya kawaida wakati wa kupumua,kushindwa kunyonya na kula,mtoto kubadilika rangi ya bluu midomo,kuumwa na tumbo na kutocheza.
Aina ya vimelea kama vile bakteria,virusi,parasite na fangasi.
Homa ya mapafu inaweza kuzuiwa kwa chanjo, lishe bora na pia mtoto kuishi katika mazingira yenye hewa safi.
Kuhimiza usafi katika makazi kama kutotumia jiko la mkaa au kuni ndani ya nyumba na uvutaji wa sigara .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni