Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2016

Tohara Kenya

Huku baadhi ya kabila nchini Kenya zikiendelea kupasha tohara wasichana,shirika la umoja wa mataifa limetaja kitendo hikikama dhuruma kwa watoto. Daktari Babatunde Osotimehin ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa UNPF ametaja ukeketaji kama kitendo cha unyama na dhuruma kwa mtoto. Alisema kuna haja ya wadau kutafuta mikakati itakayo hakikisha unyama huu imekomeshwa katika sehemu au mataifa yanaoendelea kutekeleza uovu huu,hasabara la afrika abako takwimu zinaonyesha hali ni mbaya. Mataifa ya jamhuri za kiislamu,Afrika Mashariki,Magharibi na Kusini ni baadhi ya maeneo ambayo yangali yanakubatia mila na tamaduni potovu za ukeketaji. Alisema shirika lake linatafuta mikakati na sheria ya kuhakikisha swala hili limekomeshwa kabisa. Hii ni baada ya muda wa miaka ishirini ambapo mashirika ya kiserikali nay ale ya haki za kibinadamu yakikasifu tabia ya ukeketaji barani Afrika .

TB kenya

Kiwango kikubwa cha  watu wanaogua ugonjwa wa kifua kikuu wamekuwa  wakipatikana  na Virusi Vya Ukimwi.Aidha kuchangia vifo miongoni mwa waadhiriwa. Juhudi za kupambana na TB na maambukizi ya Ukimwi zinaendelea  barani Afrika hususan nchini Kenya. Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kifua kikuu kama moja wapo wa magonjwa ambukizi yanayosababisha maafa nchini. Kesi za kifua kikuu zimeongezeka Zaidi ya mara tatu katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Mwaka wa 2015 Zaidi ya watu elfu kumi walifariki kutokana na makali ya TB. Jimbo la Pwani ya Kenya linaongoza kwa idadi ya maambukizi ya kufua kikuu huku Nairobi,Isiolo,Kisumu na Embu zikifuata. Vile vile,Majimbo ya Samburu,Tharaka,Turkana na Kirinyaga zina idadi ya azili mia 32 ya maambukizi. Kenya imekuwa mtari wa mbele kuuthibiti ugonjwa wa Tb lakini changamoto zikiwemo wagonjwa kukataa ktafuta matibabu au kukata kumeza dawa. ilibidi serikali kuweka mikakati madhubuti...

AIDS CONFERENCE DURBAN 2016

Picha
Kongamano la tano la kimataifa kuhusu ukimwi kuanza Afrika Kusini Kongamano kuhusu ukimwi liaanza   mjini Durban, Afrika Kusini. Mkutano huo wa siku tatu unawaleta pamoja wajumbe na wataalam kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni. Mkutano huo unafanyika wakati ambapo   selikali ya Kenya imejitahidi kukabiliana na makali yake.   Siku chake zilizopita, wizara ya afya Kenya, ilianzisha sera na kampeini ambayo itawasaidia wanaougua na   wanaofahamu hali yao ya HIV kupata tiba mara moja.Kampeini inayo ; anza sasa pia itawezesha watoto wanaozaliwa na virusi vya HIV kuanza matibabu mara moja.   Lakutia moyo ni kwamba   idadi ya maabukizi nchini Kenya imepungua,huku Afrika kusini hasa Durban ambapo mkutano huu unafanyika hali ikiwa sio nzuri.   Zaidi ya hayo,Utafiti unaonyesha   watu milioni 40 ulimwenguni walioambukizwa virusi vya ukimwi wanatokea barani Afrika.   Serikali ya kenya imetenga shilingi bilioni 22 kupambana na janga h...