Huku baadhi
ya kabila nchini Kenya zikiendelea kupasha tohara wasichana,shirika la umoja wa
mataifa limetaja kitendo hikikama dhuruma kwa watoto.
Daktari
Babatunde Osotimehin ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa UNPF ametaja ukeketaji kama kitendo
cha unyama na dhuruma kwa mtoto.
Alisema kuna
haja ya wadau kutafuta mikakati itakayo hakikisha unyama huu imekomeshwa katika
sehemu au mataifa yanaoendelea kutekeleza uovu huu,hasabara la afrika abako
takwimu zinaonyesha hali ni mbaya.
Mataifa ya
jamhuri za kiislamu,Afrika Mashariki,Magharibi na Kusini ni baadhi ya maeneo
ambayo yangali yanakubatia mila na tamaduni potovu za ukeketaji.
Alisema shirika
lake linatafuta mikakati na sheria ya kuhakikisha swala hili limekomeshwa
kabisa.
Hii ni baada
ya muda wa miaka ishirini ambapo mashirika ya kiserikali nay ale ya haki za
kibinadamu yakikasifu tabia ya ukeketaji barani Afrika .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni