Alhamisi, 21 Julai 2016

TB kenya



Kiwango kikubwa cha  watu wanaogua ugonjwa wa kifua kikuu wamekuwa  wakipatikana  na Virusi Vya Ukimwi.Aidha kuchangia vifo miongoni mwa waadhiriwa.

Juhudi za kupambana na TB na maambukizi ya Ukimwi zinaendelea  barani Afrika hususan nchini Kenya.

Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kifua kikuu kama moja wapo wa magonjwa ambukizi yanayosababisha maafa nchini. Kesi za kifua kikuu zimeongezeka Zaidi ya mara tatu katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Mwaka wa 2015 Zaidi ya watu elfu kumi walifariki kutokana na makali ya TB.

Jimbo la Pwani ya Kenya linaongoza kwa idadi ya maambukizi ya kufua kikuu huku Nairobi,Isiolo,Kisumu na Embu zikifuata.
Vile vile,Majimbo ya Samburu,Tharaka,Turkana na Kirinyaga zina idadi ya azili mia 32 ya maambukizi.

Kenya imekuwa mtari wa mbele kuuthibiti ugonjwa wa Tb lakini changamoto zikiwemo wagonjwa kukataa ktafuta matibabu au kukata kumeza dawa.
ilibidi serikali kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha kwa hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wanaokataa kumeza dawa.
Hata hivyo kutiwa nguvuni waliokiuka maagizo ya daktari yalikosolewa na wanaharakati wa haki za binadamu.
Hiyo pia ni changamoto kwani sheria au sera za afya na wagonjwa pia sharti kiundwe na kulindwa.

Uganda,Tanzania na Zimbabwe bado zimeonekana kushindwa kukambiliana na tishio la TB

Hivi majuzi,serikali ya Kenya  ilizidua  mradi: mulika TB,Maliza TB kama moja wapo wa juhudi za kutokomesha ugonjwa huu nchini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni