Lakini mashirika ya kiafya yanaendelea kuwahimiza akina mama
kuwanyonyesha watoto ili kuepuka maradhi na kumpa moto afya bora .
Pia ni muhimu kwa
akina mama ili kuepuka maradhi kama vile saratani ya titi au maradhi
mengine kama vile msongo wa mawazo ambao
hupata akina mama wengi baada ya kujifungia.
Kulinga na utafiti wa WHO ambayo imetolewa kwa ajili ya wiki
ya kunyonyesha duniani , ni nchi chache
tu ambazo hutekeleza mfumo wa kimataifa, unaolenga kuzuia matangazo ya lishe
mbadala kwa watoto.
Akina mama ambao hufanya kazi hasa katika mashirika tofauti
huwa na ungumu wa kupata muda wa kunyonyesha ,jambo ambalo huwachochea akina mama
kununua na kuwapa watoto wao vyakula vya mikebe.
Isitoshe,maziwa ya mama ni muhimu zaidi kumjenga motto kimwili
na pia kiakili.Hivyo basi ni vema kumnyonyesha mtoto kuliko kutengemea maziwa
ya mbadala.
Jinsi ya kunyonyesha
- Anza kunyonyesha baada ya saa moja ya kuzaa (unyonyeshaji wa mapema)
- Usimptie mtoto chochote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya kwanza (unyonyeshaji wa kipekee)
- Usimwage maziwa ya kwanza ya mama baada ya kuzaa, huwa na protini na kingamwili ambayo ni muhimu kwa mtoto mchanga. Unapaswa kumwambia mama amlishe nayo mtoto mchanga, kwa sababu ni ‘chanjo’ ya kwanza ambayo mtoto atapata.
- Keti kwa hali nzuri wakati unanyonyesha
- Hakikisha mtoto anapata vizuri matiti ya mama anaponyonya
- Hakikisha mtoto ananyonya vizuri
KAMPENI YA WHO itaendelea hadi tarehe saba Augusti kwa
malengo ya kuwaelimisha akina mama umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni