Alhamisi, 29 Septemba 2016

Saratani ya tumbo


Aliyekuwa mtangazaji mashuhuli wa kituo change habari cha Royal Media Waweru Mburu ameaga dunia.

Waweru amefariki baadaya ya kuugua saratani ya tumbo.

Alitumika kwenye Radio Citizen kwa miaka zaidi ya kumi na tano, huku akiwa na umaarufu kufuatia kipindi chake cha yaliyotendeka.

Kabla yakufa kwake hiyo jana jioni, Waweru alitangaza nia yake ya kuwania kiti cha kisiasa katika eneo la maragua, jimbo la Murang'a.


 saratani ya  tumbo ni saratani inayotokea katika mfuko was chakula unaosiaga  na kutunza chakula kwa muda. Saratani hii hutokea  katika tezi za gastric gland.
Kulingana  na takwimu za afya,saratani hii inatokea sana katika nchi za Japani na China

Kinachosababisha saratani ya tumbo?

Wataalamu wa afya hawana uhakika nini husababisha saratani hii.Hata hivyo, Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya chakula kuchomwa, chenye chumvi nyingi au kilichohifadhiwa kwenye chumvi nyingi na saratani ya tumbo..

 saratani ya tumbo  imepungua sana hasa sehemu ambapo matumizi ya friji inatumika kama njia ya kuhifadhi chakula.
 Duniani na kwa kiasi kikubwa

Kinacho changia saratani ya tumbo-gastric cancer?

Chakula chenye chumvi nyingi
Maambukizi ya bakiteria aitwaye helicobacter pyroli
Michomo ya muda mrefu tumboni(inflammations
Uvutaji wa sigara
Uvimbe kwenye kuta za tumbo kitaalamu stomach polyps

Dalili -tumbo-Gastric cancer

Kuhisi chakula kimejaa tumboni
Kichefuchefu na kutapika
Kushindwa kula chakula
Kushiba baada ya kula kidogo
Kukosa hamu ya kula
Kinyesi  cheusi au kuwa mweupe mikononi na chini ya kope kwa sababu ya upungufu wa damu
Kutapika damu
Kupungua uzito
Kuvimba tumbo aukupata uvimbe tumboni
Kuvimba mitoki san asana mitoki ya bega la kushoto na kwapani

Dalili za hatari

Kujaa maji kwenye mfuko unaofunika matumbo.
Kuziba kwa mshipa unaopitisha chakula kutoka kwenye tumbo na  husababisha chakula kujaa tumboni
Kukonda sana kutokana na saratani au kukosa hamu ya kula

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni