Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2016

TB

Tanzania imepiga hatua mbele, kwa kubuni mbinu ya kuukabili ugonjwa wa kifua kikuu, kwa kuzindua MAABARA  jijini Dar es salaam. Mradi huu utakua chini ya usimamizi wa chuo kikuu cha  Kilimo cha Sokoine. Ubunifu huu utafanywa kwa kutumia panya buku kupima sampuli za ugonjwa wa kifua kikuu (TB).Inaaminika panya mmoja ana uwezo wa kupima sampuli Mia moja katika muda wa dakika ishirini. Hatua hii imefanyika huku kukiwa na ongezeko la idadi ya wagonjwa wa kifua kikuu Tanzania. Tanzania ni miongoni nchi barani Afrika zenye maambukizi ya juu ya ugonjwa huo na kutumia njia  hii katika kupambana na ugonjwa huu itakuwa ni afueni. Wataalamu wanasema kuwa njia ya  hapo awali  ilitoa uhakika wa sampuli kwa asilimia 20 hadi 60 huko asilimia 40 hawagunduliki na hivyo kuendelea kuambukiza wengine. Daktari Georgies Mgode  anasema mradi huo wa kupima vimelea vya kifua kikuu utakutumia panya waliofunzwa. Dk.Mgode, ambaye pia ni meneja wa mradi huu, anafafanua kuwa ...

Vasectomy

Picha
Uzazi mpango Huku maisha yakiwa magumu Barani Afrika hususan Kenya, kuna haja yakufanya uzazi mpango ili kuweza kukimu mahitaji ya kila siku. Akina mama kwa muda mrefu ndiyo wenye majukumu ya kupanga uzazi Huku Akina baba wakijihuzisha n'a majukumu mengine. Lakini mambo imechukua mwelekeo mpya Huku wanaume wakiamua kupanga uzazi pia.  Haya majukumu ni ya kila mmoja, n'a ni vema kushirikiana wake kwa waume. Hii imepelekea wanaume kutafuta njia za kupanga uzazi. Njia mojawapo ya hizo ni ile ya vasectomy; kufunga mirija unaotoa mbegu za kiume. Hii ni njia ya kudumu ya kupanga uzazi. Ni majuzi tu ambapo siku ya kuadhimisha uzazi mango wa vasectomy nchini Kenya n'a pia kote duniani.  Nchini ya Kenya ilichukua fursa Hii kuelimisha jamii umuhimu wa wanaume kupanga uzazi. Kadili ya wanaume hamsini walijitokeza kufajiwa upasuaji kubana mirija yao. Hupasuaji huchukua muda wa nusu saa. Hata hivyo kuna baadhi ya wanaume wanaokosoa shughuli Hii wakisema Hii ni ...

Conjoined twins -Kenya

Picha
Wataalamu katika hospitali kuu ya Kenyatta wamefanikiwa kuwatenganisha watoto mapacha walioshikamana kwenye sehemu ya mgongo. Hiyo jana hospitali Hiyo ilitoa picha za watoto hao wakionana ana kwa ana kwa mara ya Kwanza.  Ufanishi huu umetokea baada ya miaka miwili tangu kuzaliwa kwao. Hii ni mara ya Kwanza madaktari katika hospitali Hii kuibuka na  ushindi kama huu. Pia huu ni upasuaji wa kipekee kuwahi fanyika nchini Kenya. Ilichukua muda na mpangilio wa hali ya juu kukusanya kundi la madaktari wenye ustadi katika maswala tofauti ya kiafya. Watoto hawa walizaliwa na tatizo la kiafya ambalo kulitatua kwa haraka lingehatarisha maisha yao. Hâta hivyo, kulikuwa na matumaini kuwa mafanikio ya kuwatenganisha yangepatikana. Watoto Blessing na Favor walizaliwa miaka miwili iliyopita katika hospitali ya Mtakatifu Theresa,  Kiirua katika Jimbo la Meru. Baadaya ya madaktari kushindwa kutatua hali yao kutokana na ukosefu wa vifaa au mashine za kisasa, w...