Huku maisha yakiwa magumu Barani Afrika hususan Kenya, kuna haja yakufanya uzazi mpango ili kuweza kukimu mahitaji ya kila siku.
Akina mama kwa muda mrefu ndiyo wenye majukumu ya kupanga uzazi Huku Akina baba wakijihuzisha n'a majukumu mengine.
Lakini mambo imechukua mwelekeo mpya Huku wanaume wakiamua kupanga uzazi pia.
Haya majukumu ni ya kila mmoja, n'a ni vema kushirikiana wake kwa waume.
Hii imepelekea wanaume kutafuta njia za kupanga uzazi.
Njia mojawapo ya hizo ni ile ya vasectomy; kufunga mirija unaotoa mbegu za kiume.
Hii ni njia ya kudumu ya kupanga uzazi.
Ni majuzi tu ambapo siku ya kuadhimisha uzazi mango wa vasectomy nchini Kenya n'a pia kote duniani.
Nchini ya Kenya ilichukua fursa Hii kuelimisha jamii umuhimu wa wanaume kupanga uzazi.
Kadili ya wanaume hamsini walijitokeza kufajiwa upasuaji kubana mirija yao.
Hupasuaji huchukua muda wa nusu saa.
Hata hivyo kuna baadhi ya wanaume wanaokosoa shughuli Hii wakisema Hii ni tabia ambapo haiabatani na destuli za kiafrika.
Wanasema haya ni mambo ya kizungu ambayo yanafaa kupakia na wazungu tu.
Wengine nao wanatoa maoni tofauti.
Wanaonelea ni vema kupanga uzazi wa vasectomy kwani unasaidia kupunguza majukumu, huku watoto wachache wakipata mahitaji yao bila shinda yeyote.
Wanasema ni vema wanaume kuwasaidia wake wao kupanga familia.
Uchumi umezorota, watoto na jamaa kwa jumla wana mahitaji mengi .Wasipopanga uzazi basi wazazi watakuwa wanawaacha watoto wao kuumia.
Jambo muhimu la kufahamu ni kuwa njia hii;
*Haipunguzi hamu ya kufanya ngono
*Haizuii maambukizi ya magonjwa ya zinaa.Hivyo basis ni vema kuchukua tahathali.
*Hali hii ni ya kudumu.Haitawezekana tena kupata watoto baada ya operesheni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni