Jumatatu, 28 Novemba 2016
TB
Tanzania imepiga hatua mbele, kwa kubuni mbinu ya kuukabili ugonjwa wa kifua kikuu, kwa kuzindua MAABARA jijini Dar es salaam. Mradi huu utakua chini ya usimamizi wa chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine.
Ubunifu huu utafanywa kwa kutumia panya buku kupima sampuli za ugonjwa wa kifua kikuu (TB).Inaaminika panya mmoja ana uwezo wa kupima sampuli Mia moja katika muda wa dakika ishirini.
Hatua hii imefanyika huku kukiwa na ongezeko la idadi ya wagonjwa wa kifua kikuu Tanzania.
Tanzania ni miongoni nchi barani Afrika zenye maambukizi ya juu ya ugonjwa huo na kutumia njia hii katika kupambana na ugonjwa huu itakuwa ni afueni.
Wataalamu wanasema kuwa njia ya hapo awali ilitoa uhakika wa sampuli kwa asilimia 20 hadi 60 huko asilimia 40 hawagunduliki na hivyo kuendelea kuambukiza wengine.
Daktari Georgies Mgode anasema mradi huo wa kupima vimelea vya kifua kikuu utakutumia panya waliofunzwa.
Dk.Mgode, ambaye pia ni meneja wa mradi huu, anafafanua kuwa panya hao wana uwezo wa kubaini harufu ya vimelea vya ugonjwa huo ndani ya sekunde.
Aidha, alisema mbinu hii itakuwa mwafaka kwa wagonjwa na watafiti pia. Ishitoshe, muda utapunguka. Hapo awali kupima sampuli 100 kwa maabara zinazotumia hadubini kulichukua muda wa sikuu nne.Lakini sasa mgonjwa atapata majibu ndani ya siku moja na kuanza tiba.
“Ni kweli hawa panya wana faida kubwa kwenye ugunduzi wa vimelea vya ugonjwa wa TB, kwa sababu wana uwezo ndani ya sekunde wakabaini maambukizi ya kwa mgonjwa wakati mtu wa maabara anatumia zaidi ya siku moja kupata majibu,” alieleza Dk Mgode.
Alisema maabara nyingine ya panya buku iko mjini Morogoro ambayo hutumika kupima sampuli mbalimbali kutoka hospitali 28 nchini. Tangu mradi huo uanze kazi mwaka 2008 zaidi ya sampuli 380,000 zimeshapimwa.
Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP), Dk Allan Tarimo alisema Tanzania ni moja ya nchi zenye maambukizi ya juu ya ugonjwa wa kifua kikuu barani Afrika ikiorodheshwa ya nne huku kimataifa ikiwa nafasi ya sita.
Hakika hii ni hatua kubwa ya kuokoa maisha ya wagonjwa na kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo ambao ni changamoto Tanzania.
Kinaya ni kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO)) linasema, kwa siku moja mtaalamu wa maabara anatakiwa kupima wagonjwa 20 tu wa kifua kikuu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni