Dolutegravir(DTG) dawa ya VVU
Shirika la Afya Duniani (WHO) limependekeza dawa ya Dolutegravir(DTG) katika mapambano yake dhidi ya virusi vya Ukimwi,licha ya dawa hiyo kushukiwa kuwa na madhara kwa akina mama waja wazito. Pendekezo hili limetolewa siku mmoja baadaya ya shirika hilo ,kuchapisha taarifa inayoonyesha kuwa mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi bado yanaendelea. WHO inapendekeza matumizi ya Dolutegravir(DTG) kama njia ya kwanza na ya pili ya matibabu kwa watu wote,wakiwemo akina mama wajawazito na pia wenye uwezo wakupata ujauzito. Tafiti za awali, zilitia shaka uwezekano wa kuwepo kwa uhusiano kati ya dawa ya DTG na tatizo linalosababisha watoto kuzaliwa na tundu kwenye uti wa mgongo na ubongo,yaani Spinal bifida. Tatizo hili hutokea punde tu mama anapopata ujauzito huku akitumia dawa ya DTG. Kenya ni miongoni mwa nchi ambazo zilitoa tahadhari dhidi ya matumizi ya dawa ya DTG baadaya ya utafiti uliofanywa nchini Botswana kuonyesha kuwa dawa h...